MUWSA kutoa Sh Milioni 2 kwa watakaotaja wezi wa mita za maji Moshi

MUWSA kutoa Sh Milioni 2 kwa watakaotaja wezi wa mita za maji Moshi

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA) imeeleza kuwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka huu, mita za maji 266 zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 37.2 zimeibwa hali inayopelekea hasara kwa mamlaka hiyo na usumbufu kwa wateja wake.

Hoja ya wizi wa Mita ~ Tatizo la Wizi wa Mita za Maji na pendekezo kwa mamlaka husika

Akizungumza leo Machi 23, 2026, Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Flora Nguma amesema kuwa maeneo yanayo ongoza kwa hujuma hizo wa wizi wa mita za maji ni pamoja na Mamlaka ya Mji mdogo wa Himo, Kata ya Makuyuni, Kata ya Majengo, Mwika Kaskazini na Mwika kusini hali inayopelekea Wananchi kukosa huduma ya maji ilihali mamlaka hiyo ina uwezo wa kuhudumia Wananchi.

Amesema kuwa katika kuhakikisha wezi hao wa mita za maji wanakamatwa ili kukomesha tabia hiyo, Mamlaka hiyo itatoa kiasi cha Shilingi Milioni mbili kwa Mwananchi atakaye toa taarifa za uhakika kuhusu wanao hujumu na kuiba mita hizo.

"Mamlaka imekuja na kitita cha shilingi Milioni mbili kwa Mwananchi yeyote atakaye toa taarifa za kuthibitika dhidi ya mtu anayeiba au kununua mita hizo", alisisitiza Nguma.

Amesema kuwa mbali na mita hizo kuibiwa hujuma nyingine ni wizi wa mifuniko ya chemba za maji safi na taka, pamoja na viungio vya mita za maji na kwamba Mamlaka hiyo ilitoa uwezeshaji kwa vikundi vya ulinzi shirikishi wa vifaa ili kukamata wezi hao, jambo ambalo bado halijasaidia huku Serikali ikipata hasara kubwa na wananchi wakiendelea kuteseka kwa kukosa maji.

Awali Mamlaka hiyo ilitoa taarifa kuwa katika kipindi cha miaka mitatu mita 543 ziliibiwa maeneo tofauti Wilaya Moshi na kusabibishia mamlaka hiyo hasara kubwa ya mamilioni ya pesa.

Pia soma: KERO - Wizi wa Mita za Maji Moshi unaendelea, wanaoiba wanapeleka wapi? Bora Mita zikae ndani ya uzio
 
Hizo mita huwa zina issue gani? Vyuma chakavu? Na za plastic wanabeba?
 
waongeze dau, mita zimeibiwa za sh milioni 37 na ujinga, dau la kuwataja wezi ni milioni mbili bila hata ushee. acheni utani na kazi za watu
 
Back
Top Bottom