"Unajua inasikitisha sana. Kuna muda inabidi tucheke japo havichekeshi. Watu wanajiita wanaharakati, wanajiita wakombozi wa taifa japo taifa letu limeshakombolewa toka mwaka 1961, tukapata uhuru tukawa taifa huru. Kuna watu wanajiita wanaharakati wanataka kulikomboa taifa.
Lakini nataka niwakumbushe hapa, unajua lazima tuwakumbushe; hata Musa alipotaka kwenda kulikomboa taifa la Israel hakutuma barua ya posta. Musa alimvaa Farao, hakutuma barua ya posta, alikwenda kukabiliana na changamoto zote zilizopo kwa Farao. Ejapo kuwa alitumwa na Mungu.
Ila hawa waliotumwa na wazungu, wanaolipwa, waitwa wenyewe... wanatuma barua ya posta. Watanzania tuamke. Kama umetumwa na Mungu atakupa ujasiri wa kuja. Ili taifa liwateue, hili taifa limeshakombolewa na waasisi wetu—ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuna Mzee Abeid Karume, kuna kina mama zetu kina Bibi Titi Mohamed, watu mbalimbali kina Mzee Sykes wameshanipigania hili taifa, wala halihitaji harakati ya kukombolewa. Limeshakombolewa.
Na kina Nyerere wakati walikomboa hawakutuma barua ya posta, ujue. Waliwafuata wazungu, 'tunataka taifa letu'. Na kufikia na mambo mengine, na leo tuko huru. Kama mnataka kulikomboa taifa, msitume barua ya posta, njooni, Hata Musa hakutuma barua kwa Farao, alimvaa, akaenda kwa Farao japo alitumwa na Mungu.
Ila ninyi mliotumwa na wazungu... mnaogopa, mnachochea tu, mnatuma barua ya posta."