Muziki kutoka nchini Zaire (sasa ni D.R.C) uliwezaje kutamalaki na kupendwa sana hapa Tanzania ilhali tumepakana na jirani wengine takribani 6?

Mziki wao ni mzuri kiasi kwamba hata kama hufahamu kilingala ile lugha yao wanayo itumia ni lazima utafurahia tu na kama kungekuwa na Kombe la Dunia la Muziki basi DRC kila mara wangekuwa wanashinda wao tu na hilo Kombe kubaki huko huko kwao Milele.
Hakika DRC ndio mabingwa wa muziki hapa Afrika. Tanzania tunapaswa kujitahidi na kuja kuwa kama wao.
 
Hili swali ni gumu kidogo maana nakumbuka miaka ya 70 wakati nipo sec tulikuwa tunazisililiza sana
Pia kwenye radio walikuwa wanaweka sana labda wazaire wa kuja ndio walikuja na miziki yao
Halafu zamani Radio za Africa zilikuwa pia zinapayikana kwa urahisi ikiwa na maana tulikuwa more advanced kiliko sasa ( [emoji24])
Nakumbuka hata graduation zilikuwa bila miziki yao hapakaliki
Daa umenifanya nisilikilize Mbale na (Kiam)Memi pamoja na Kasongo maana zile bits sio za dunia hii
 
Ila Muziki wa Nigeria ni kama sampling ya muziki wa Congo.

e.g Sikiliza Chop Money ya P Square.
 
Mkuu, au wewe ndiye yule anayejiita Manji wa Muziki kule TBC FM (Radio Tanzania)?
 
Kulikuwa na nyimbo nyingi sana za mtindo wa twist za akina Fadhili William, Edward Masengo, Mwenda John Bosco, Haji Fundi Konde, Equator Sound Boys na wengine wengi.
Wakati huo na sisi mziki wetu ulikuwa unavuma sana huko Kenya ama la?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…