Nakubariana na maneno yako ya mwanzo kama ulivyo andika. Lakini pia nakuomba ili ujiridhishe maendeleo yanayo fanywa Chato ufanye utafiti Chato imeanzia wapi! ukipata historia ya Chato, utaunga mkono maendeleo ya sasa. Kwa ufupi Chato ilikuwa imeterekezwa na mkoa wa Kagera hivyo huduma nyingi hazikupatikana hapo mpaka uende Bukoba, na kwenda huko mpaka upite Biharamulo au urudi mpaka Geita (Nyuma) ili uweze kubahatisha usafiri kwenda kuhudumiwa Bukoba. Mpaka tunapojadili hapa kuna mafaili ya serikali ambayo yako Archive Bukoba Kagera na hayajarudishwa Geita. Hili lilikuwa ni shinikizo mojawapo la kutaka Chato na Geita ziwe Mkoa mpya.
Wakazi wa Chato waliteseka sana - inashangaza sana kuona wananchi waliofaidi keki ya taifa miaka mingi wanakasirika kuwa sasa hivi Chato wamepata jengo moja la CRDB, taa moja ya trafic barabarani, hoteli moja***, uwanja wa ndege, mbuga ya wanyama moja, shule moja, barabara ya lami moja, zahanati moja, uwanja utajengwa mmoja, Chuki hii lakini, kwanini? Kama ni sababu ya upinzani, kweli hapa utaabulia kura ngapi!