Na Bwanku Bwanku.
Leo Jijini Mwanza kumefanyika tukio kubwa la kihistoria katika Nchi yetu ambapo Meli kubwa na ya Kisasa sana ya MV Mwanza hatimaye imeshushwa kwenye maji kwenye Ziwa Victoria kuelekea kuanza kutoa huduma kuwahudumia wananchi kwenye eneo zima la Maziwa Makuu.
Akizungumza kwenye hafla ya ushushaji wa Meli hiyo majini leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli nchini Ndugu Eric Hamissi amesema ujenzi wa Meli hii kubwa ya Kisasa ulianza mwaka 2019 na wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani Machi 2021, ujenzi wa reli hii ulikuwa umefikia chini ya asilimia 40, lakini ndani ya muda mfupi wa Uongozi wa Rais Dkt. Samia tayali ujenzi wake umefikia asilimia 82, ikiwa hatua za mwisho kukamilika.
Ujenzi wa Meli hii kubwa umeigharimu Serikali Bilioni 109 na itakuwa na uwezo wa kubeba watu 1,200 na Tani 400 kwa mpigo na kurahisisha usafiri na kuchochea uchumi eneo la Bandari ya Mwanza kuelekea Bukoba na eneo zima la Maziwa Makuu kuelekea Uganda na Kenya.
Meli hii ina hospitali ndani, ina ghorofa 4 na lifti za kurahisisha kupanda ghorofa ndani na kuingilia , ina uwezo wa kupambana na hali mbaya ya hewa, ina migahawa na restaurant za kisasa ndani pamoja na eneo la kucheza mziki ili kuondoa uchovu kwa wasafiri, ina ingine kubwa ya kisasa ya akiba na mengine mengi.
#HakunaKilichosimama
#KaziInaendelea