Uchaguzi 2020 Mvua iliwanufaisha Profesa Kitila na Dkt. Magufuli

Juma Katolila

New Member
Joined
Jun 1, 2020
Posts
4
Reaction score
10
Wadau,

Leo mvua kubwa inanyesha Dar es Salaam. Hata hivyo, haikuwazuia Wananchi wa Majimbo ya Ubungo na Kibamba kwenda kumsikiliza Rais John Magufuli na wagombea Ubunge wa majimbo hayo kwenye Mkutano wa hadhara pale Mburahati.

Mkutano ulikuwa na sababu zote za kutofanikiwa. Kwanza ulipangwa asubuhi saa mbili, siku ya kazi, mvua ilikuwa kubwa na mambo mengine madogomadogo.

Cha ajabu, watu hawakujali mvua. Uwanja ukajaa watu kiasi kwamba Rais Magufuli alizungumza kwa hisia sana kwenye Mkutano huo. Alisema hajawahi kuona mapenzi ya aina ile.

Mkutano huo ungeahirishwa ungekuwa pasua kichwa kubwa kwa wagombea Kitila Mkumbo wa Ubungo na Issa Mtemvu wa Kibamba.

Kusingekuwa na Mvua, mkutano ule ungefanyika na kumalizika kama mingine ya kawaida. Mvua imebadilisha mambo.

Ikamfanya Rais Magufuli alazimike kuahidi kitu palepale uwanjani. Ikafanya ghafla maelfu yale ya watu waliolowa watengeneze bond na Rais na wabunge wao.

Kwa hiyo Kitila akaambiwa aseme anataka nini. Naye, bila kusita, akasema. Moja kwa moja, wananchi wakajua sasa wana mtu ambaye ana click na Rais.

Kama Rais Magufuli ni pipa, basi Kitila ndiye mfuniko wake. Kama mvua isingenyesha Dar leo, huenda hili tusingeliona.

INAWEZEKANA, kwamba mvua hii ya leo, ndiyo imempa Ubunge Profesa Kitila Mkumbo.
 
Bukombe muda mchache uliopita...

1602602002206.jpeg
 
Mjomba Magu katupa pole Ubungo kwa kutengwa kimaendeleo.Kumbe Ubungo imepuuzwa kwa miaka kibao sababu eti ya kuwa chini ya upinzani.Tokea enzi za Mkapa waliipuzia .Hata miundo mbinu tunayoiona ni kwasababu ni gateway ya kwenda pahala pengine.
 
Mvua imempa Ubunge Kitila kilaini kabisa

Leo mvua kubwa inanyesha Dar es Salaam. Hata hivyo, haikuwazuia wananchi wa majimbo ya Ubungo na Kibamba kwenda kumsikiliza Rais John Magufuli na wagombea Ubunge wa majimbo hayo kwenye Mkutano wa hadhara pale Mburahati.

Back
Top Bottom