Mfafanulie swali alilouliza acheni ujeuri wenu wa kielimu,Tambua kuna wengi awajui sio yeye tu je uoni kama ukimfafanulia anaweza kwenda kueneza ufahamu kwa watoto wake au kwa watu waliomzunguka,? Kwanini Watanzania tupo hivi badala ufundishe mtu aelewe uongeze watu waelewa, wewe na elimu yako kubwa unamkandamiza na kejeli nyingi na lugha kali, kama ni bwege, mtoro, atavuna mabua. Inasikitisha sana .. Sasa ulichomsaidia hapo ni nini? Watu wote wangekuwa wabinafsi kama wewe unafikiri ungejua kusoma,, hata hizo Google ulizopitia wewe ni watu wenye ufahamu wa kujua kwamba kuna watu watahitaji msaada wa kufahamu jambo moja au lingine na ndio maana hata wewe uliweza kuambiwa kwamba kuna Google unaweza kutafuta kitu fulani au habari fulani ukaipata.., Ninachotaka kusema kwa kifupi ukiona mtu kauliza swali, kama unajua jibu lake mjibu au mfafanulie kama ujibu piga kimya. Hakuna swali la kijinga dunia ..ujinga ni ujinga na swali ni swali. Siku njema ndugu.