Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mvua iliyonyesha kwa takribani dakika 10 jijini Mbeya imeacha kilio kwa wakazi wa Mtaa wa Nzovwe baada ya maji kuingia kwenye nyumba na kusomba bidhaa za wafanyabiashara, zikiwemo kuku.
Mvua hiyo ya mawe iliyonyesha leo Jumanne, Novemba 3, 2026, imesababisha mafuriko yaliyoathiri makazi na shughuli za biashara katika eneo hilo.
Mwananchi imetembelea eneo hilo na kushuhudia wakazi wakiwa wamejikusanya katika makundi, huku baadhi wakijitahidi kuondoa maji yaliyochanganyika na tope yaliyovamia nyumba zao.
Wakizungumzia athari za mvua hiyo, baadhi ya wakazi hao wamesema nyumba kadhaa zimeharibika, huku wafanyabiashara wakipata hasara baada ya bidhaa zao kusombwa na maji, zikiwemo kuku.
View: https://www.instagram.com/reel/DfSIvZ8C-9F/