Mvua za El nino: Serikali inasubiri nini kufunga shule

Mvua za El nino: Serikali inasubiri nini kufunga shule

Kama Dar hali ni hiyo huku mikokani ndo itakuwa balaa
Hakika shule za msingi zifungwe mapema kuepusha madhara kea watoto wadogo
 
Waache wanyeshewe, nimevuka mto mabhale (kwa mabhale) miaka ya tisini acheni kudekeza vitoto vyenu
 
Mi mwenyewe nimelowa sana Leo wakati wa kurudi home...mvua gani haisikii hata mwamvuli....imeharibu mwamvuli wangu umegeuka juu kwa upepo mkali....kesho siendi kazini😖
Umeloa hadi ndani?
 
Halafu mtu gari lote yupo peke yake hata kuchukua watoto watatu hataki anaona kabisa wanaloa ukiuliza watachafua.
Vimefundishwa vikatae lift unaweza kutaka kumsaidia mtoto anakataa bora tuwe tunawaacha tu siku kuna kitoto kilikuwa na mwenzake kikasema lift nikasimama niwapakie mmoja akakataa nikambeba mwenzake hivyo ni kuwaacha tu
 
Kwa hali ya hewa inavyoendelea hivi sasa nashauri shule za Dar zifungwe kwa muda hadi January 2024.

Watoto wakae majumbani na familia zao ili kuepusha maafa zaidi na MADHARA yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazoendelea jijini Dar es Salaam.
 
wewe ni nani hadi utoe ushauri mkubwa kihivyo. acha wenye vyeo vyao wafanye kazi zao
 
Andaa mtoto kwa ajili ya barabara, usipende kuandaa barabara tu kwa ajili ya mtoto.

Mnunulie makoti mabuti na maboya ya kuogeleaa aelee tu akisombwa na maji. Ongezea sasa na filimbi ya kuombea msaada (mfundishe kuitumia tu)😆😅😅😅😅😅😅

On a serious note lakini tujitahidi kuwaandaa watoto kuweza kuhimili mikikimkiki ya maisha kuliko kutaka kusawazisha kila aina ya changamoto kwa ajili yao. Jikague na kasome suala la helicopter parents.

Na kama hali ni ngumu sana, basi wafunge kweli na hilo jambo ni kiotomati tu hali itaonesha
 
Back
Top Bottom