Mvua zinazonyesha haziingizi Maji kwenye Mabwawa ya Umeme, acheni kulaumu kuhusu Mgawo
Mkuu umesahau, walisema tatizo la umeme nchi hii ni mvua kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, wakahamia kwenye gas na hadithi tamu tamu. Leo hii hakuna anayezungumzia umeme wa gas tena. Na ukiuliza hilo wanapiga chenga ya hatari. Watoto wa mjini wanasema wamejizima data.
Cc Tlaatlaah
cc: Mama Samia
TAKUKURU
TANESCO a.k.a. Shirika la hasara Tanzania
 
Hii ndio Taarifa mpya kutoka Tanesco , kwamba hizo mvua mnazoona zinanyesha haziwezi kupunguza mgawo wa umeme kwa vile maji ya mvua hizo hayaingii kwenye mabwawa hayo , haijulikani kama mabwawa hayo yamepigwa Bati juu yake au La

Na mnaambiwa zaidi mvua hizo zinaharibu miundo mbinu na kuongeza matatizo .

TANESCO imesema mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini hususani katika ukanda wa Pwani na ukanda wa Ziwa Victoria, mtiririko wa maji yake hauelekei viliko vyanzo vya uzalishaji wa umeme vya Mtera, Kihanzi na Kidatu.

Mkurugenzi wa TANESCO, Eng. Gissima Nyamo-Hanga amesema mvua hizo zimeleta athari katika miundombinu ya shirika katika baadhi ya maeneo, hivyo kuongeza changamoto katika upatikanaji wa umeme.
Kama hayaingii mabwawani,natuambiwe wanakunywa viboko,mamba,samaria tembo,simba ,chui au swala wa nyikani🤔
 
Jamani wenzangu mnabonyeza wapi kupata hizi hadithi.
Naona mnafaidi.😁
 
Hivi kina mwamposa hawawezi kuisaidia hi inchi kimiujiza mambo yake yakakaa sawa??!!😶😫
 
Kweli hawa TANESCO akili zao zinawatosha wenyewe. Yaani kutokuwepo na mgao wa umeme miaka sita ya JPM hapakuwa na mgao wa umeme, baada ya kufariki maji ya mvua yakabadili uelekeo nje ya mabwawa ya uzalishaji umeme! Stupid kabisa
 
Back
Top Bottom