Mvutano Mirathi ya Mengi wapamba moto. Abdiel & Benjamin wapinga kutupwa maombi yao na Mahakama ya Rufani

sajo

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
3,474
Reaction score
6,195
Mtoto mkubwa wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, marehemu Reginald Mengi amefungua maombi Mahakama ya Rufani akitaka ipitie upya uamuzi wake wa kutupilia mbali hoja zao za kutaka mahakama hiyo isisikilize shauri lililofunguliwa na mjane wa tajiri huyo, Jacqueline Ntuyabaliwe anayepinga kutenguliwa kwa wosia wa mume wake.

Machi mwaka jana, Mahakama Kuu, Dar es Salaam, ilitengua wosia wa mwisho wa Mengi baada ya kuyakataa maombi yaliyofunguliwa na watu wanne waliokuwa wakitaka mahakama hiyo iwathibitishe kuwa wasimamizi wa mirathi ya mfanyabiashara huyo.

Mtoto huyo wa Mengi, Abdiel na kaka wa tajiri huyo, Benjamin Mengi walipinga maombi hayo wakidai wosia huo uliompa Jacqueline karibu mali zote za mfanyabiashara huyo haukuwa halali. Jaji Yose Mlyambina alikubaliana na watoto wa Mengi na kutengua wosia uliodaiwa kuandikwa na baba yao.

Katika wosia huo, Mengi ambaye alikuwa mmiliki wa kampuni za IPP alidaiwa alimrithisha mali zake zote Jacqieline na watoto pacha aliozaa naye---Jayden Kihoza Mengi na Ryan Saashisha Mengi na kuwaweka kando watoto aliozaa na mke wake wa kwanza, Mercy Mengi ambaye walitengana. Mercy alifariki dunia Novemba 2018.

Mahakama Kuu ilikubaliana na hoja za watoto wakubwa wa Mengi kuwa baba yao alikuwa amepoteza uwezo wa kiakili wa kuandika wasia halali kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yakimkabili. Mahakama hiyo iliridhika kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwamba marehemu alipatwa na ugonjwa wa kiharusi tangu Oktoba 2016 na hakupata nafuu hadi mauti yalipomfika.

“Hii ina maana kuwa uwezo wake wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi uliathirika na kumfanya asiweze kuelewa maana ya uamuzi sahihi wa usimamizi wa mirathi yake,” ilisema mahakama.

Vita mpya ya mirathi

Kutokana na uamuzi huo, Jacqueline alifungua maombi Mahakama ya Rufani akiitaka ipitie upya na iubatilishe uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutengua wosia wa mume wake uliomilikisha karibu mali zote za tajiri huyo. Hatua hiyo haikufawafurahisha watoto wa Mengi ambao waliweka pingamizi wakitaka mjane huyo asisikilizwe. Katika moja ya hoja zao, walidai Jacqueline hakuwa na uhalali wa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kwa njia ya kuomba mapitio Mahakama ya Rufani badala ya kukata rufaa. Pia walidai maombi hayo hayakuwa sawa kisheria kwa kutoambatanishwa na nyaraka muhimu.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani iliyatupilia mbali mapingamizi hayo ikisema kwa kuwa Jacqueline hakuwa sehemu ya kesi ya msingi iliyofunguliwa Mahakama Kuu alikuwa na uwezo wa kufungu mapitio katika mahakama hiyo. Wakasema hata mapungufu yaliyoainishwa kwenye maombi yake hayakuwa na athari katika kesi aliyofungua, hivyo kutoa kibali kwa shauri alilofungua kusikilizwa.

Watoto wa Mengi wapinga

Hivi karibuni, Abdiel na Benjamin wamefungua maombi katika Mahakama ya Rufaa wakitaka mahakama hiyo ya juu nchini ipitie upya uamuzi wake. Wanapinga uamuzi wa Mahakama ya Rufani kutupilia mbali pingamizi lao dhidi ya maombi ya mapitio yaliyofunguliwa na mjane huyo akipinga hukumu ya Mahakama Kuu, iliyoukataa wosia huo.

Pamoja na mambo mengine, kina Abdiel katika maombi yao hayo wanadai kuwa uamuzi huo wa mahakama hiyo hauzingatia misingi ya kisheria. Mawakili wa Jacqueline wameiomba mahakama izitupilie mbali hoja hizo wakidai hazina mashiko kisheria.

Tayari Mahakama ya Rufani imesikiliza hoja za watoto wa Mengi na ndugu zao na itatoa notisi ya kuzijulisha pande zote tarehe ya uamuzi.

Mengi alifariki dunia Mei 2, 2019 akiwa nchini Dubai alipokuwa anapatiwa matibabu.

Chanzo: James Magai - Gazeti la Mwananchi, Machi 02, 2022
 
Nikisoma habari za hizi seke seke za bilionea mengi kwenye mirathi. Na zile za bilionea msuya kwenye mirathi.

Nagundua kuna makosa makubwa matajiri wanafanya kwenye malezi na mirathi.

Ni wakati sasa kila ukoo kuwa na katiba yao binafsi ya ukoo.. ambayo inakuwa imeeleza utaratibu wa kila kitu kwenye ukoo wao. Mtu anapoolewa ama kuoa huo ukoo apewe aisome kwanza katiba ya ukoo mpya kabla hajafunga ndoa. Na katiba hiyo isajiliwe kabisa kisheria.

Hizi ndoa za kikristo hizi ni za kizungu ukiziendekeza zinaamisha mali kwenye ukoo kama utani na kuzipeleka ukoo mwingine.

Mfano baba wa bilionea msuya. Mwanae amefariki na wengine wameuwawa kisa mirathi. Na bado mali za ukoo wao zinasimamiwa na kaka wa mke wa mtoto wao. Eti kisa mke yupo jela kwa kumuua wifi yake ila mali za ukoo wa msuya zinasimamiwa na kaka wa mke kutokea ukoo wa mrita.

Haya mambo wahindi na waarabu wapo makini nayo sana. Ndio maana hawapotezi utajiri wao vizazi na vizazi
 
Nikisoma habari za hizi seke seke za bilionea mengi kwenye mirathi. Na zile za bilionea msuya kwenye mirathi.

Nagundua kuna makosa makubwa matajiri wanafanya kwenye malezi na mirathi.

Ni wakati sasa kila ukoo kuwa na katiba yao binafsi ya ukoo.. ambayo inakuwa imeeleza utaratibu wa kila kitu kwenye ukoo wao. Mtu anapoolewa ama kuoa huo ukoo apewe aisome kwanza katiba ya ukoo mpya kabla hajafunga ndoa. Na katiba hiyo isajiliwe kabisa kisheria.

Hizi ndoa za kikristo hizi ni za kizungu ukiziendekeza zinaamisha mali kwenye ukoo kama utani na kuzipeleka ukoo mwingine.

Mfano bilionea msuya. Mwanae amefariki na wengine wameuwawa kisa mirathi. Na bado mali za ukoo wao zinasimamiwa na kaka wa mke wa mtoto wao. Eti mke yupo hela ila mali za ukoo wa msuya zinasimamiwa na kaka wa mke kutokea ukoo mwa mrita.

Haya mambo wahindi na waarabu wapo makini nayo sana. Ndio maana hawapotezi utajiri wao vizazi na vizazi
Hilo jambo unalosema liliweza na linaweza kutekelezeka kupitia WOSIA, sasa shida ni kuwa Sheria inaruhusu kutikisa (challenge) uhalali wa huo wosia na kupitia hapo ndio meza zinapopinduliwa.

Ama watu wanaghushi wosia ( wanatengeneza wa kwao na kuusema ni wa marehemu) ama wosia halali uliotolewa na marehemu unapigwa na sababu za kisheria na kuonekana ni batili.
 
Hilo jambo unalosema liliweza na linaweza kutekelezeka kupitia WOSIA, sasa shida ni kuwa Sheria inaruhusu kutikisa (challenge) uhalali wa huo wosia na kupitia hapo ndio meza zinapopinduliwa. Ama watu wanaghushi wosia ( wanatengeneza wa kwao na kuusema ni wa marehemu) ama wosia halali uliotolewa na marehemu unapigwa na sababu za kisheria na kuonekana ni batili.

Wosia unakuwa na utata mwingi sababu unafichwa fichwa. Wosia hauwi wazi ili ukoo mzima uusome wakati mwenye mali yupo hai.

Katiba inakuwa wazi kila mtu wa kwenye ukoo anaisoma na anakuwa na nakala yake. Hata watoto wakizaliwa wanapewa nakala zao. Na mke au mume akifunga ndoa huo ukoo anapewa nakala yake
 
Mtoto mkubwa wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, marehemu Reginald Mengi amefungua maombi Mahakama ya Rufani akitaka ipitie upya uamuzi wake wa kutupilia mbali hoja zao za kutaka mahakama hiyo isisikilize shauri lililofunguliwa na mjane wa tajiri huyo, Jacqueline Ntuyabaliwe anayepinga kutenguliwa kwa wosia wa mume wake. Machi mwaka jana, Mahakama Kuu, Dar es Salaam, ilitengua wosia wa mwisho wa Mengi baada ya kuyakataa maombi yaliyofunguliwa na watu wanne waliokuwa wakitaka mahakama hiyo iwathibitishe kuwa wasimamizi wa mirathi ya mfanyabiashara huyo.

Mtoto huyo wa Mengi, Abdiel na kaka wa tajiri huyo, Benjamin Mengi walipinga maombi hayo wakidai wosia huo uliompa Jacqueline karibu mali zote za mfanyabiashara huyo haukuwa halali. Jaji Yose Mlyambina alikubaliana na watoto wa Mengi na kutengua wosia uliodaiwa kuandikwa na baba yao.

Katika wosia huo, Mengi ambaye alikuwa mmiliki wa kampuni za IPP alidaiwa alimrithisha mali zake zote Jacqieline na watoto pacha aliozaa naye---Jayden Kihoza Mengi na Ryan Saashisha Mengi na kuwaweka kando watoto aliozaa na mke wake wa kwanza, Mercy Mengi ambaye walitengana. Mercy alifariki dunia Novemba 2018. Mahakama Kuu ilikubaliana na hoja za watoto wakubwa wa Mengi kuwa baba yao alikuwa amepoteza uwezo wa kiakili wa kuandika wasia halali kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yakimkabili. Mahakama hiyo iliridhika kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwamba marehemu alipatwa na ugonjwa wa kiharusi tangu Oktoba 2016 na hakupata nafuu hadi mauti yalipomfika.

“Hii ina maana kuwa uwezo wake wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi uliathirika na kumfanya asiweze kuelewa maana ya uamuzi sahihi wa usimamizi wa mirathi yake,” ilisema mahakama.

Vita mpya ya mirathi

Kutokana na uamuzi huo, Jacqueline alifungua maombi Mahakama ya Rufani akiitaka ipitie upya na iubatilishe uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutengua wosia wa mume wake uliomilikisha karibu mali zote za tajiri huyo. Hatua hiyo haikufawafurahisha watoto wa Mengi ambao waliweka pingamizi wakitaka mjane huyo asisikilizwe. Katika moja ya hoja zao, walidai Jacqueline hakuwa na uhalali wa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kwa njia ya kuomba mapitio Mahakama ya Rufani badala ya kukata rufaa. Pia walidai maombi hayo hayakuwa sawa kisheria kwa kutoambatanishwa na nyaraka muhimu.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani iliyatupilia mbali mapingamizi hayo ikisema kwa kuwa Jacqueline hakuwa sehemu ya kesi ya msingi iliyofunguliwa Mahakama Kuu alikuwa na uwezo wa kufungu mapitio katika mahakama hiyo. Wakasema hata mapungufu yaliyoainishwa kwenye maombi yake hayakuwa na athari katika kesi aliyofungua, hivyo kutoa kibali kwa shauri alilofungua kusikilizwa.

Watoto wa Mengi wapinga

Hivi karibuni, Abdiel na Benjamin wamefungua maombi katika Mahakama ya Rufaa wakitaka mahakama hiyo ya juu nchini ipitie upya uamuzi wake. Wanapinga uamuzi wa Mahakama ya Rufani kutupilia mbali pingamizi lao dhidi ya maombi ya mapitio yaliyofunguliwa na mjane huyo akipinga hukumu ya Mahakama Kuu, iliyoukataa wosia huo. Pamoja na mambo mengine, kina Abdiel katika maombi yao hayo wanadai kuwa uamuzi huo wa mahakama hiyo hauzingatia misingi ya kisheria. Mawakili wa Jacqueline wameiomba mahakama izitupilie mbali hoja hizo wakidai hazina mashiko kisheria.

Tayari Mahakama ya Rufani imesikiliza hoja za watoto wa Mengi na ndugu zao na itatoa notisi ya kuzijulisha pande zote tarehe ya uamuzi.

Mengi alifariki dunia Mei 2, 2019 akiwa nchini Dubai alipokuwa anapatiwa matibabu.

Chanzo: James Magai - Gazeti la Mwananchi, Machi 02, 2022
Huyu mzee mbona alikuwa anaonekana yupo makini sana hadi akatunga na kitabu.
 
Wosia unakuwa na utata mwingi sababu unafichwa fichwa. Wosia hauwi wazi ili ukoo mzima uusome wakati mwenye mali yupo hai.

Katiba inakuwa wazi kila mtu wa kwenye ukoo anaisoma na anakuwa na nakala yake. Hata watoto wakizaliwa wanapewa nakala zao. Na mke au mume akifunga ndoa huo ukoo anapewa nakala yake
Ni jambo zuri mkuu, ingawa jmbo hilo litahitaji mabadiliko ya sheria ya mirathi - ni la msingi sana.
 
Nikisoma habari za hizi seke seke za bilionea mengi kwenye mirathi. Na zile za bilionea msuya kwenye mirathi.

Nagundua kuna makosa makubwa matajiri wanafanya kwenye malezi na mirathi.

Ni wakati sasa kila ukoo kuwa na katiba yao binafsi ya ukoo.. ambayo inakuwa imeeleza utaratibu wa kila kitu kwenye ukoo wao. Mtu anapoolewa ama kuoa huo ukoo apewe aisome kwanza katiba ya ukoo mpya kabla hajafunga ndoa. Na katiba hiyo isajiliwe kabisa kisheria.

Hizi ndoa za kikristo hizi ni za kizungu ukiziendekeza zinaamisha mali kwenye ukoo kama utani na kuzipeleka ukoo mwingine.

Mfano baba wa bilionea msuya. Mwanae amefariki na wengine wameuwawa kisa mirathi. Na bado mali za ukoo wao zinasimamiwa na kaka wa mke wa mtoto wao. Eti kisa mke yupo jela kwa kumuua wifi yake ila mali za ukoo wa msuya zinasimamiwa na kaka wa mke kutokea ukoo mwa mrita.

Haya mambo wahindi na waarabu wapo makini nayo sana. Ndio maana hawapotezi utajiri wao vizazi na vizazi

Kichwa cha chini kikisimamishwa vizuri cha juu kinalala haya ndo matokeo, unaweza hata kujitoa wewe urithi ukifa mkeo akuchukue.
 
Kuna mdau alianzisha uzi humu akasema wale wadada wapo watano wote wapo kimkakati wamejilengesha na kuolewa na wenye pesa yaani,

JACQUELINE
FARAJA
NANSI

wengine wawili nimewasahau mmoja ishatimia bado hao wengine na ukichunguza ni kweli kwa kinachoendelea sasa hivi ila wachaga sio wakuoa wale.
 
Nikisoma habari za hizi seke seke za bilionea mengi kwenye mirathi. Na zile za bilionea msuya kwenye mirathi.

Nagundua kuna makosa makubwa matajiri wanafanya kwenye malezi na mirathi.

Ni wakati sasa kila ukoo kuwa na katiba yao binafsi ya ukoo.. ambayo inakuwa imeeleza utaratibu wa kila kitu kwenye ukoo wao. Mtu anapoolewa ama kuoa huo ukoo apewe aisome kwanza katiba ya ukoo mpya kabla hajafunga ndoa. Na katiba hiyo isajiliwe kabisa kisheria.

Hizi ndoa za kikristo hizi ni za kizungu ukiziendekeza zinaamisha mali kwenye ukoo kama utani na kuzipeleka ukoo mwingine.

Mfano baba wa bilionea msuya. Mwanae amefariki na wengine wameuwawa kisa mirathi. Na bado mali za ukoo wao zinasimamiwa na kaka wa mke wa mtoto wao. Eti kisa mke yupo jela kwa kumuua wifi yake ila mali za ukoo wa msuya zinasimamiwa na kaka wa mke kutokea ukoo mwa mrita.

Haya mambo wahindi na waarabu wapo makini nayo sana. Ndio maana hawapotezi utajiri wao vizazi na vizazi
Ila ukisoma ule wosia ni wa kitoto sana hata mtoto mdogo anayejua kusoma anaweza kuona makosa yaani atakayepinga apewe buku aisee wachaga mpo vizuri kwenye hyo sekta.
 
Huyu mzee mbona alikuwa anaonekana yupo makini sana hadi akatunga na kitabu.

Hako kamwanamke kametumia uzuri wake kummaliza mzee wa watu. Na sasa kanataka kamiliki na kampuni zake, as if kalimsaidia kwenye kuzitafuta.

Binafsi naungana na watoto wakubwa wa marehemu. Wapambanie haki yao mpaka mwisho. Na ikishindikana kabisa, basi ni bora wakakosa wote.
 
Wosia unakuwa na utata mwingi sababu unafichwa fichwa. Wosia hauwi wazi ili ukoo mzima uusome wakati mwenye mali yupo hai.

Katiba inakuwa wazi kila mtu wa kwenye ukoo anaisoma na anakuwa na nakala yake. Hata watoto wakizaliwa wanapewa nakala zao. Na mke au mume akifunga ndoa huo ukoo anapewa nakala yake
Kuweka wosia wazi ni hatari mno...
Jaribu uwaishwe mbele za haki
 
Kuweka wosia wazi ni hatari mno...
Jaribu uwaishwe mbele za haki

Waarabu na wahindi mbona hawapelekani mbele za haki mapema.

Wosia siupendi sababu unakuwa na maficho maficho kwa ndugu zako wa ukoo.

Tazama mirathi ya bilionea mengi na hata bilionea msuya. Zote zina wosia. Lakini bado ugomvi mkubwaa mpaka wanauana.

Wahindi na waarabu matajiri wanarithisishana mapema na bado utajiri haupotei
 
Kuna mdau alianzisha uzi humu akasema wale wadada wapo watano wote wapo kimkakati wamejilengesha na kuolewa na wenye pesa yaani,

JACQUELINE
FARAJA
NANSI

wengine wawili nimewasahau mmoja ishatimia bado hao wengine na ukichunguza ni kweli kwa kinachoendelea sasa hivi ila wachaga sio wakuoa wale.
Kwa Nancy hakuna kitu[emoji848]
 
Back
Top Bottom