Mvutano Mirathi ya Mengi wapamba moto. Abdiel & Benjamin wapinga kutupwa maombi yao na Mahakama ya Rufani

Mvutano Mirathi ya Mengi wapamba moto. Abdiel & Benjamin wapinga kutupwa maombi yao na Mahakama ya Rufani

Jack naye awe na aibu sasa, binafsi namuona kama mtu mwenye tamaa na ujinga mwingi.

Yaani jitu limepambana na mke wake miaka yote mpaka wanafikisha over 60yrs pamoja na mitoto mikubwa na mihangaiko yao yote ya kuutafuta utajiri wewe umeingia tu una miaka haifiki hata mitatu kwenye ndoa mtu akiwa na utajiri wake unataka mirathi mali zote....DUNIA INA MAMBO SANA.... hapa Jack anataka kudhulumu jasho la watu bure kabisa.

Anachostahili ni kusomeshewa watoto na matunzo ya watoto ikiwa pamoja na kuishi nyumba nzuri watoto, budget ya kula siku, shule five stars vyote vikilipwa na IPP group... watoto wawe na shares kidogo baafa ya majibu ya DNA....

Yeye aende akafanye kazi ikiwezekana apewe offer ya Kazi IPP group....otherwise atakuwa anasumbuliwa na njaa tu aka anatafuta mteremko..
 
Yule Mzee alichoharibu kama kweli ni yeye mwenyewe ndiye kaandika ule wosia ni kuwabagua wale watoto wake wakubwa kwamba wasipate chochote kwenye urithi wake, yeye kama alitaka kuwanyima angeweza kusema tu warithi nguo au kitu kingine chochote kisichokuwa na thamani kubwa basi.

Lakini kuwanyima kabisa ndipo alipokosea.
 
Wenzetu waasia mambo ya urithi wamejitahidi kuyaweka vizur

Mengi uhusiano wake na familia sijui ulikuaje ila kwa umri wake watt wake ndio walitakiwa wawe ndio wasimamizi wakuu yy akiwa pemben kama mshauri

Ila cha kuhuzunisha na miaka yake ile huku akitetemeka alikua akionekana kwenye tv akipambania co utadhani watt hana
 
Nikisoma habari za hizi seke seke za bilionea mengi kwenye mirathi. Na zile za bilionea msuya kwenye mirathi.

Nagundua kuna makosa makubwa matajiri wanafanya kwenye malezi na mirathi.

Ni wakati sasa kila ukoo kuwa na katiba yao binafsi ya ukoo.. ambayo inakuwa imeeleza utaratibu wa kila kitu kwenye ukoo wao. Mtu anapoolewa ama kuoa huo ukoo apewe aisome kwanza katiba ya ukoo mpya kabla hajafunga ndoa. Na katiba hiyo isajiliwe kabisa kisheria.

Hizi ndoa za kikristo hizi ni za kizungu ukiziendekeza zinaamisha mali kwenye ukoo kama utani na kuzipeleka ukoo mwingine.

Mfano baba wa bilionea msuya. Mwanae amefariki na wengine wameuwawa kisa mirathi. Na bado mali za ukoo wao zinasimamiwa na kaka wa mke wa mtoto wao. Eti kisa mke yupo jela kwa kumuua wifi yake ila mali za ukoo wa msuya zinasimamiwa na kaka wa mke kutokea ukoo wa mrita.

Haya mambo wahindi na waarabu wapo makini nayo sana. Ndio maana hawapotezi utajiri wao vizazi na vizazi
Waarabu/Wahindi pia hawaoi ngozi pendwa kwa kadhia Kama hizi
 
Bila kumsahau the late bilionea Mrema wa Ngurdoto, Naura Spring, na Impala hotels Arusha.
 
Naona huyo Jack anajitahidi apelekwe kuzimu, hio ni dhuluma ya wazi...yaani kukata viuno kidogo tu kwa mzee kwa vi miaka vichache basi anataka urithi wote.

Wakimpeleleka kuzimu ni haki yake sio kwa dhuluma hio.
 
Wosia unakuwa na utata mwingi sababu unafichwa fichwa. Wosia hauwi wazi ili ukoo mzima uusome wakati mwenye mali yupo hai.

Katiba inakuwa wazi kila mtu wa kwenye ukoo anaisoma na anakuwa na nakala yake. Hata watoto wakizaliwa wanapewa nakala zao. Na mke au mume akifunga ndoa huo ukoo anapewa nakala yake
Watu wanaogopa kufa kwa kuweka wosia wazi, limtu linajua kitarithi mali kinakutanguliza na cynide
 
Wenzetu waasia mambo ya urithi wamejitahidi kuyaweka vizur
Mengi uhusiano wake na familia sijui ulikuaje ila kwa umri wake watt wake ndio walitakiwa wawe ndio wasimamizi wakuu yy akiwa pemben kama mshauri
Ila cha kuhuzunisha na miaka yake ile huku akitetemeka alikua akionekana kwenye tv akipambania co utadhani watt hana

Watoto wake walikua wanasimamia hizo Company miaka yote bila Mzee kuwepo na wao ndio walikua signatories

Walikua wana uwezo wa kumpa hela Mzee au kumyima baada ya kumuona anapotea na kuwaongezea madeni kwa sababu ya michepuko

Mdangaji hakua na taarifa nyingi za maisha ya hiyo familia anaenda kudondokea pua tena hii ni rufaa ya Mia mbili kyln anakata🤓🤓🤓🤓
 
Nikisoma habari za hizi seke seke za bilionea mengi kwenye mirathi. Na zile za bilionea msuya kwenye mirathi.

Nagundua kuna makosa makubwa matajiri wanafanya kwenye malezi na mirathi.

Ni wakati sasa kila ukoo kuwa na katiba yao binafsi ya ukoo.. ambayo inakuwa imeeleza utaratibu wa kila kitu kwenye ukoo wao. Mtu anapoolewa ama kuoa huo ukoo apewe aisome kwanza katiba ya ukoo mpya kabla hajafunga ndoa. Na katiba hiyo isajiliwe kabisa kisheria.

Hizi ndoa za kikristo hizi ni za kizungu ukiziendekeza zinaamisha mali kwenye ukoo kama utani na kuzipeleka ukoo mwingine.

Mfano baba wa bilionea msuya. Mwanae amefariki na wengine wameuwawa kisa mirathi. Na bado mali za ukoo wao zinasimamiwa na kaka wa mke wa mtoto wao. Eti kisa mke yupo jela kwa kumuua wifi yake ila mali za ukoo wa msuya zinasimamiwa na kaka wa mke kutokea ukoo wa mrita.

Haya mambo wahindi na waarabu wapo makini nayo sana. Ndio maana hawapotezi utajiri wao vizazi na vizazi
Sio kama naupendelea Uislamu ila Uislamu umeeleza vzr sana mambo ya mirathi na ukifuata sheria hasaa hakuna atakaelalamika.
kwenye Uislamu ni jambo dogo sana hilo
 
Sio kama naupendelea Uislamu ila Uislamu umeeleza vzr sana mambo ya mirathi na ukifuata sheria hasaa hakuna atakaelalamika.
kwenye Uislamu ni jambo dogo sana hilo
Lakini sasa cha kushangaza sasa, wengi wa wanufaika wa mali za marehemu aliyekua muislamu, yaani watoto wa marehemu huwa hawataki mirathi itoke kwa sheria ya kiislamu, wanataka itoke kwa sheria ya mirathi (PAEA Cap 352)
 
Mtoto mkubwa wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, marehemu Reginald Mengi amefungua maombi Mahakama ya Rufani akitaka ipitie upya uamuzi wake wa kutupilia mbali hoja zao za kutaka mahakama hiyo isisikilize shauri lililofunguliwa na mjane wa tajiri huyo, Jacqueline Ntuyabaliwe anayepinga kutenguliwa kwa wosia wa mume wake. Machi mwaka jana, Mahakama Kuu, Dar es Salaam, ilitengua wosia wa mwisho wa Mengi baada ya kuyakataa maombi yaliyofunguliwa na watu wanne waliokuwa wakitaka mahakama hiyo iwathibitishe kuwa wasimamizi wa mirathi ya mfanyabiashara huyo.

Mtoto huyo wa Mengi, Abdiel na kaka wa tajiri huyo, Benjamin Mengi walipinga maombi hayo wakidai wosia huo uliompa Jacqueline karibu mali zote za mfanyabiashara huyo haukuwa halali. Jaji Yose Mlyambina alikubaliana na watoto wa Mengi na kutengua wosia uliodaiwa kuandikwa na baba yao.

Katika wosia huo, Mengi ambaye alikuwa mmiliki wa kampuni za IPP alidaiwa alimrithisha mali zake zote Jacqieline na watoto pacha aliozaa naye---Jayden Kihoza Mengi na Ryan Saashisha Mengi na kuwaweka kando watoto aliozaa na mke wake wa kwanza, Mercy Mengi ambaye walitengana. Mercy alifariki dunia Novemba 2018. Mahakama Kuu ilikubaliana na hoja za watoto wakubwa wa Mengi kuwa baba yao alikuwa amepoteza uwezo wa kiakili wa kuandika wasia halali kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yakimkabili. Mahakama hiyo iliridhika kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwamba marehemu alipatwa na ugonjwa wa kiharusi tangu Oktoba 2016 na hakupata nafuu hadi mauti yalipomfika.

“Hii ina maana kuwa uwezo wake wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi uliathirika na kumfanya asiweze kuelewa maana ya uamuzi sahihi wa usimamizi wa mirathi yake,” ilisema mahakama.

Vita mpya ya mirathi

Kutokana na uamuzi huo, Jacqueline alifungua maombi Mahakama ya Rufani akiitaka ipitie upya na iubatilishe uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutengua wosia wa mume wake uliomilikisha karibu mali zote za tajiri huyo. Hatua hiyo haikufawafurahisha watoto wa Mengi ambao waliweka pingamizi wakitaka mjane huyo asisikilizwe. Katika moja ya hoja zao, walidai Jacqueline hakuwa na uhalali wa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kwa njia ya kuomba mapitio Mahakama ya Rufani badala ya kukata rufaa. Pia walidai maombi hayo hayakuwa sawa kisheria kwa kutoambatanishwa na nyaraka muhimu.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani iliyatupilia mbali mapingamizi hayo ikisema kwa kuwa Jacqueline hakuwa sehemu ya kesi ya msingi iliyofunguliwa Mahakama Kuu alikuwa na uwezo wa kufungu mapitio katika mahakama hiyo. Wakasema hata mapungufu yaliyoainishwa kwenye maombi yake hayakuwa na athari katika kesi aliyofungua, hivyo kutoa kibali kwa shauri alilofungua kusikilizwa.

Watoto wa Mengi wapinga

Hivi karibuni, Abdiel na Benjamin wamefungua maombi katika Mahakama ya Rufaa wakitaka mahakama hiyo ya juu nchini ipitie upya uamuzi wake. Wanapinga uamuzi wa Mahakama ya Rufani kutupilia mbali pingamizi lao dhidi ya maombi ya mapitio yaliyofunguliwa na mjane huyo akipinga hukumu ya Mahakama Kuu, iliyoukataa wosia huo. Pamoja na mambo mengine, kina Abdiel katika maombi yao hayo wanadai kuwa uamuzi huo wa mahakama hiyo hauzingatia misingi ya kisheria. Mawakili wa Jacqueline wameiomba mahakama izitupilie mbali hoja hizo wakidai hazina mashiko kisheria.

Tayari Mahakama ya Rufani imesikiliza hoja za watoto wa Mengi na ndugu zao na itatoa notisi ya kuzijulisha pande zote tarehe ya uamuzi.

Mengi alifariki dunia Mei 2, 2019 akiwa nchini Dubai alipokuwa anapatiwa matibabu.

Chanzo: James Magai - Gazeti la Mwananchi, Machi 02, 2022
Utajiri autafute mwingine kuminyana wafanye wengine.....

Ama kweli BURE NA MAISHA KITONGA ni mtihani sana.....

#Tafuta Pesa Ya Halali Na Uitumie Kwa Kujitanguliza binafsi halafu ndio wafuatie wengine
 
Lakini sasa cha kushangaza sasa, wengi wa wanufaika wa mali za marehemu aliyekua muislamu, yaani watoto wa marehemu huwa hawataki mirathi itoke kwa sheria ya kiislamu, wanataka itoke kwa sheria ya mirathi (PAEA Cap 352)
Maelekezo na utekelezaji ni vitu viwili tofauti.....

Hata wasipotekeleza ,sheria ya dini itabaki palepale kwani wako wanaoitekeleza iwe wanaishi Luanda ,Syria ,Germany ama Mauritius!
 
Kwangu Mimi jambo kubwa la kujifunza hapa ni kuishi na mwanamke. Ukipata Hela ukiwa umeshaoa, jitahidi Sana kumu upgrade mkeo awe na ka exposure Fulani hivi.

Na kama unataka kumbato mwanamke yeyote na unajua una Hela tafuta mwanamke ambaye level yake inaendana na wewe.

Hakuna kitu kibaya kama unakuwa na hela halafu unazaa na vilaza case study nzuri ni yule Bilionea wa Arusha mwenye mahotel.
 
Watoto wake ndio walikua wanasimamia hizo Company miaka yote bila Mzee kuwepo na wao ndio walikua signatories

Walikua wana uwezo wa kumpa hela Mzee au kumyima baada ya kumuona anapotea na kuwaongezea madeni kwa sababu ya michepuko

Mdangaji hakua na taarifa nyingi za maisha ya hiyo familia anaenda kudondokea pua tena hii ni rufaa ya Mia mbili kyln anakata🤓🤓🤓🤓
Sasa ilitakiwa iwe wazi kwenye umiliki
Yaani nani ana miliki kipi na kipi
 
Back
Top Bottom