Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kwamba hata yule kijana aliyekamatwa Rungwe kwa kosa la kuipiga kiberiti picha ya Rais Samia, hana kosa lolote na hata wakamataji hawajui wampachike kesi gani, maana kwa katiba ya Tanzania kitendo kile ni sawa na mtu kuokota makaratasi ili awashie mkaa kwenye jiko lake.
Inadaiwa kukamatwa kwake kumesababishwa na mihemko tu na fikra duni za viongozi wa Mbeya
=========
Ni siku tatu tangu Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limkamate Shadrack Chaula (24), kijana anayetuhumiwa kuchoma moto picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, suala hilo limeibua mvutano wa kisheria, ikielezwa hakuna sheria iliyovunjwa.
Akizungumza na Mwananchi jana Julai 3, 2024 kuhusu kosa la kijana huyo na lini atafikishwa mahakamani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema jukumu lao liliishia kumkamata suala la kupelekwa mahakamani linabaki kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
“Siwezi kusema ni lini atapelekwa mahakamani, kazi yetu ilikuwa ni kumkamata, Ofisi ya Mashtaka ndiyo itaandaa mashtaka kwa kuangalia ushahidi na kuonyesha ni vifungu gani vya sheria mtuhumiwa amekiuka,” amesema.
Suala hilo pia limeibua mjadala kwenye mitando ya kijamii na miongoni mwa waliolijadili ni Wakili Peter Kibatala aliyeandika ujumbe kupitia ukurasa wake, na baadaye alipotafutwa na Mwananachi kuufafanua, amesema amewaelekeza mawakili wiwili kwenda kutoa msaada wa kisheria kwa kijana huyo.
“Hatutaingilia maamuzi ya mkuu wa mkoa aliyetaka kijana huyo ahojiwe, lakini atakapopelekwa mahakamani ana haki ya kupata msaada wa kisheria, ndiyo maana niliwagiza mawakili wenzangu wawili kwenda kumsaidia kijana huyo,” amesema.
Wakili wa kujitegemea, Philip Mwakilima akizungumza na Mwananchi amesema hakuna sheria wala kifungu kinachoonyesha kuchoma au kutochoma picha ya kiongozi huyo ni kosa na hakuna athari yoyote kwa jamii.
(Imeandikwa na Waandishi Wetu)
Mwananchi
Pia soma:Kuelekea 2025 - Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake