my friend, republic hawajawahi kukosa kosa la kushitaki.
kitu nawashauri vijana, siasa sio fujo, nasema hivi kwasababu huwezi kushindana kwenye fujo na mtu mwenye dola na pesa. ccm wana dola na pesa. wewe huna polisi, huna TISS huna jeshi utashindana nao kwa manguvu? si utaumia tu.
Pili, harakati zenu fanyeni kwa busara, hekima na maarifa. Hoja dhidi ya hoja, acheni matusi. Kijana wetu sativa tunamwonea huruma sana, ni mdogo, hana hata career, anatafutiza tu chumba cha kupanga, ila mdomoni alikuwa na matusi mazito sana sana, hafanani na alivyo. sababu hiyo alijitengenezea maadui wengi, hakwenda kwa hekima na busara, hata Mungu kuamwokoa basi tu kwasababu yeye hana Mungu, ni mtu mwenye mdomo mchafu, tujifunze, na yeye ajifunze, jenga hoja, acha matusi.
someni mazingira, Tanzania sio kenya, na sio marekani ambako uhuru wako wa kujieleza upo asilimia mia. marekani unaweza kuchoma ramani ya nchi, au picha ya rais, hawakufanyi kitu. hapa ukichoma utakamatwa na utafungwa. kwa akili tu, badilisheni tactic za mapambano yenu kulingan ana mazingira. huyo dogo amechoma picha ya rais, kwa bongo icho kitu hakikubaliki.
kenya waliandamana, waliharibu vitu, waliwachezea polisi, walifanya yote wapendavyo, na hawakufanywa kitu sana. Tanzania chezea polisi utajua mwenyewe, ndio maana tunasema cheza mziki kulingana na rythm yake.
chadema acheni matusi, chadema acheni matusi, chadema acheni matusi, nimewataja mara tatu. jengeni hoja, mjibiwe kwa hoja, maguvu hamtaweza kwasababu watanzania ni waoga na pia ninyi hamna dola, mnaumiza vijana wetu bure kwa maslahi ya matumbo yenu.