Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Nimecheka wakili anauliza maswali, kachoma picha iliyopigwa au kuchorwa na nani ambae sasa analalamika? Na mnajuaje picha iliyochomwa inafanana na Samia hadi mseme kachoma picha ya Samia, toa ushahidi😀😀😀Choma tu, kinachokatazwa ni kunyofoa picha za kampeni na kuziharibu wakati kampeni zikiendelea
Halafu nimemwona Kamanda wa Polisi Mbeya ni mtupu aliposema, sie tumemkamata tunasubiri DPP atuambie tumemkamata kwa kuvunja sheria ipi! Yaani Polisi wa Tanzania bwana, ovyo sana. Sasa kwa nini Mkuu wa Mkoa aliposema kamkamate hamkuuliza haya maswali? Kuna siku Kamanda wa Polisi ataambiwa amkamate mwanamke kwa sababu kamkataa mkuu wa mkoa. Wawe na ujasiri wa kuuliza unatutuma tumkamate huyu mtu kwa kuvunja sheria gani na kushauri kama ni sawa kumkamata au la. Polisi wasiwe wanaamrishwa na wanasiasa kama hawana akili kichwani, ni roboti tu.
Hivi kama mimi ni msanii, nikachora picha ya Samia, lakini watu wakasema nimekosea macho sijayafanya marembo kama yalivyo ya Samia, na kidevu sijaweka cha mfuto kama chake, nikaamua kuichoma ili nichore picha nyingine, nitashitakiwa kwa kosa la kuchoma picha ya Samia?