Halafu boni mwenyewe yupo smart mno kichwani
Wafute hiyo kesi, maana bon yai akija na vielelezo itakua shida
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Halafu boni mwenyewe yupo smart mno kichwani
Wewe KENGE acha uogauoga!Tutumie Mitandao vizuri sio kupost vitu ambavyo huna uhakika navyo Mchuma Janga hula na wakwao
Changamoto inakuja kwa hizi simu tunaunlock kwa finger print na unakuta hukuLog out account zako.Nakumbusha tu, mahakama ikitoa AMRI kwamba u-LOGIN kwenye akaunti yako ya mtandano, log in mara kadhaa kwa 'password' ya uongo halafu usema UMESAHAU 'password'.
Kisheria, kama DPP atasema mtuhumiwa UNAKUMBUKA password, basi yeye (DPP) atatakiwa KUTHIBITISHA hilo, la sivyo itabaki kuwa TUHUMA tu dhidi yako.
Hakimu naye, hana MAMLAKA kisheria & hawezi kukulazimisha ukumbuke jambo fulani kichwani mwako kwa sababu FAHAMU ni jambo la Muumba. Kesi inakuwa imefia hapo.
Good Night.
Baba Mwita X
Marketing strategy yakeBoni Yai. Nachekaga sana hili jina, linafurahisha. 😁
Boniface Jacob ameweza kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Septemba 19,2024,toka akamatwe hapo jana katika mgahawa wa Golden Fork, Sinza.
Hati ya Mashtaka ya kesi inayomkabili Boniface Jacob inaeleza kuwa anatuhumiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, kifungu cha 16.
Katika shitaka la kwanza linaeleza kuwa Boniface Jacob mnamo Septemba 12, 2024, akiwa Dar es Salaam alichapisha taarifa za uongo zikieleza kuwa: "...Mafwele anatuhumiwa na familia nyingi kama mtu ambaye ameshiriki mauaji kwa moja katika kuwapoteza ndugu wa baadhi ya familia zao; kupotea kwa Mfanyabiashara Mussa mziba, Kupotea kwa Deo Mugasa, Kupotea kwa Adinani Hussein Mbezi, Kupotea kwa vijana watano wa Aggrey.." katika mtandao wa X (zamani uliojulikana kama X0 akitumia jina la Boniface Jacob@ExmayorUbungo akikusudia kuudanganya umma.
Na shitaka la pili pia linahusu kuchapisha taarifa za uongo kinyume ambapo linaeleza: Boniface Jacob mnamo Septemba 14,2024, alichapisha taarifa za uongo zilizosema;"....Mkawasifia maRCO wanaouzuia uhalifu kwa kutenda uhalifu,...Bali Ma RCO waliojua kuteka, kukamata, kupiga watuhumiwa risasi, kuwafunga tape, kuwafunga mifuko ya nailoni usoni na kisha kutupa miili ya watuhumiwa ndiyo wanaojua kazi ya upolisi..." katika mtandao wa X (zamani uliojulikana kama Twitter) akitumia jina la Boniface Jacob@ExmayorUbungo akikusudia kuudanganya umma.
Jacob aliyakana mashtaka yote mawili katika kesi hiyo anayowakilishwa na Mawakili watatu akiwemo Peter Kibatala na Hekima Mwasipu.
"Upande wa mashtaka umeleta maombi wanataka Mahakama imuamuru Boni awape maafisa wa polisi wapelelezi, wachunguzi uwezo wa kuingia kwenye simu yake na mtandao wa X. Kwa hiyo tumepinga vikali maombi hayo tumesema hayana sababu , wala msingi wowote kisheria," alieleza Wakili Kibatala akizungumzia mwenendo wa kesi hiyo.
Upande wa mashtaka pia umeiomba Mahakama isimpe Boniface Jacob dhamana kwa kueleza kuwa usalama wake upo hatarini. Jambo ambalo mawakili wake wameeleza halina msingi wowote wa kisheria.
Maamuzi kuhusu dhamana ya Boniface Jacob yanategemewa kutolewa mnamo Septemba 23, 2024, saa tano asubuhi.
- Soma Pia:
Jeshi la Polisi: Tumemkamata Boniface Jacob kwa makosa ya Jinai anayotuhumiwa nayo
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga kutoa uamuzi wa dhamana Boniface Jacob, septemba 23, 2024
View: https://youtu.be/OJBOxYR_98Y?si=LwP_XXF_niPDsoaD
Huyo Mafwele ndio angetakiwa kumfungulia kesi ya defamation huyo Boni Yao…sijajua serikali inaingiaje hapa au tu ni Kwa sababu mafweke ni mtumishi wa serikali?Nilisema kwenye ile kesi yake nyingine akiwa na Malisa, pia nasema tena kwenye hii pia. Kesi za mambo ya kwenye tovuti za kijamii isiyo ya kikoa cha Bongo (.tz), Polisi haitakaa itoboe.
Mwishowe wataikimbia tu kesi kama wanavyoikimbia ile nyingine. Twitter wanatoaje ushahidi utakaotosha kumfunga Boniyai? Ndiyo maana walijaribu kupora password yake.
Kwa kuwa uporaji wa password haukufanikiwa, na kumfunga pia hakutafanikiwa kamwe hadi na hii kesi waikimbie pia. Ni kupoteza muda na pesa tu za umma.
Maneno ya mitandaoni hujibiwa kwa utendaji tu uliotukuka na sio kesi za namna hii za kushindwa kabla hata haijaanza. Ni laana kutumia mgogo wa siasa kuficha uzembe wa polisi kiutendaji.
Ova
Pia mumeo akamatwe kwa kuuza madawa ya kulevyaHuyu afungwe, na pia awekewe utakatishaji isiyo na dhamana
Polisi wanajuaje kama Mafwele hahusiki?Tufike mwisho siyo katikati ya kesi mwendesha mashtska hana nia ya kuendelea na kesi aiseee.
Wao jamhuri wanajuaje kama Mafwele hahusiki? hawa wanajua fika kuwa Mafwele ndiyo mhusika no 1Kwanini huyo Mafwele asijitokeze mwenyewe kumfungulia kesi Bonny.
Huyo Mafwele kwani hayupo?
Wanajua ukweli tu akijitokeza hadharani na kwa joto la kesi hii camera na mitandao ya kijamii basi wengi sana watamtambua wajihi wake vizuri hivyo huenda hata waliowahi kuteswa naye au kufanyiwa mateso kwa amri yake watajitokeza .
Maana mahakamani hataingia kwa kujificha kama anayotekeleza maovu yake huko mafichoni.
Kichaa wa ccmHuyu afungwe, na pia awekewe utakatishaji isiyo na dhaman
Mkuu, fanya ukamsaidie Maranja Masese kulisha kuku wa BoniKichaa wa ccm
Sitaki kesi iishie kati hiyo ya Boni yai, km ile ya Mbowe. Nataka tusome na kujua PGO zoote safari hii.Polisi wanajuaje kama Mafwele hahusiki?