much know
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 11,461
- 17,183
Ndo aje navyo asije na debe tupu ili kujipatia millage kisiasaWafute hiyo kesi, maana bon yai akija na vielelezo itakua shida
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndo aje navyo asije na debe tupu ili kujipatia millage kisiasaWafute hiyo kesi, maana bon yai akija na vielelezo itakua shida
Swali la msingi sanaHoja ya kwanza: Mafwele ndo kashitaki au jamhuri inashitaki Kwa niaba ya Mafwele!?
Mafwele hatuhumiki? Mafwele ni chombo Gani katika nchi?
Hata mimi limesababisha nikitafakari mara kadhaaBoni Yai. Nachekaga sana hili jina, linafurahisha. 😁
Nakumbusha tu, mahakama ikitoa AMRI kwamba u-LOGIN kwenye akaunti yako ya mtandano, log in mara kadhaa kwa 'password' ya uongo halafu usema UMESAHAU 'password'.
Kisheria, kama DPP atasema mtuhumiwa UNAKUMBUKA password, basi yeye (DPP) atatakiwa KUTHIBITISHA hilo, la sivyo itabaki kuwa TUHUMA tu dhidi yako.
Hakimu naye, hana MAMLAKA kisheria & hawezi kukulazimisha ukumbuke jambo fulani kichwani mwako kwa sababu FAHAMU ni jambo la Muumba. Kesi inakuwa imefia hapo.
Good Night.
Baba Mwita X
HAKUNA shida kabisaAjiandae kukaa mahabusu muda mrefu
Uko sahihi kabisa. Halafu mbaya zaidi ni kuwa huyu Mafwele ni mtuhumiwa wa mauaji tangu zamani sana. Wananchi hawajaanza leo. Nakumbuka ni tangu kabla ya Magufuli hajawa rais. Amekaa Arusha, Mwanza na sasa Dar na kote anatuhumiwa.Nilisema kwenye ile kesi yake nyingine akiwa na Malisa, pia nasema tena kwenye hii pia. Kesi za mambo ya kwenye tovuti za kijamii isiyo ya kikoa cha Bongo (.tz), Polisi haitakaa itoboe.
Mwishowe wataikimbia tu kesi kama wanavyoikimbia ile nyingine. Twitter wanatoaje ushahidi utakaotosha kumfunga Boniyai? Ndiyo maana walijaribu kupora password yake.
Kwa kuwa uporaji wa password haukufanikiwa, na kumfunga pia hakutafanikiwa kamwe hadi na hii kesi waikimbie pia. Ni kupoteza muda na pesa tu za umma.
Maneno ya mitandaoni hujibiwa kwa utendaji tu uliotukuka na sio kesi za namna hii za kushindwa kabla hata haijaanza. Ni laana kutumia mgogo wa siasa kuficha uzembe wa polisi kiutendaji.
Ova
Amygdala, ni Sehemu ya ubongo inahusika na hofu, (threats), ukiwa na hofu eneo hilo la ubongo husababisha binadamu aahirishe kufikiri mambo mengine, akili ya binadamu ina maajabu yake
Ccm na policcm ni watekaji na wauaji na ushahidi upo. Nguvu ya ccm ili iwepo ni lazima watumie njia za panya kama hizo za kuyadhibiti wapinzani.Tutumie Mitandao vizuri sio kupost vitu ambavyo huna uhakika navyo Mchuma Janga hula na wakwao
Ndio nguvu yenu ya kujenga hoja zilipoishia.Huyu afungwe, na pia awekewe utakatishaji isiyo na dhamana
Boniface Jacob ameweza kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Septemba 19,2024,toka akamatwe hapo jana katika mgahawa wa Golden Fork, Sinza.
Hati ya Mashtaka ya kesi inayomkabili Boniface Jacob inaeleza kuwa anatuhumiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, kifungu cha 16.
Katika shitaka la kwanza linaeleza kuwa Boniface Jacob mnamo Septemba 12, 2024, akiwa Dar es Salaam alichapisha taarifa za uongo zikieleza kuwa: "...Mafwele anatuhumiwa na familia nyingi kama mtu ambaye ameshiriki mauaji kwa moja katika kuwapoteza ndugu wa baadhi ya familia zao; kupotea kwa Mfanyabiashara Mussa mziba, Kupotea kwa Deo Mugasa, Kupotea kwa Adinani Hussein Mbezi, Kupotea kwa vijana watano wa Aggrey.." katika mtandao wa X (zamani uliojulikana kama X0 akitumia jina la Boniface Jacob@ExmayorUbungo akikusudia kuudanganya umma.
Na shitaka la pili pia linahusu kuchapisha taarifa za uongo kinyume ambapo linaeleza: Boniface Jacob mnamo Septemba 14,2024, alichapisha taarifa za uongo zilizosema;"....Mkawasifia maRCO wanaouzuia uhalifu kwa kutenda uhalifu,...Bali Ma RCO waliojua kuteka, kukamata, kupiga watuhumiwa risasi, kuwafunga tape, kuwafunga mifuko ya nailoni usoni na kisha kutupa miili ya watuhumiwa ndiyo wanaojua kazi ya upolisi..." katika mtandao wa X (zamani uliojulikana kama Twitter) akitumia jina la Boniface Jacob@ExmayorUbungo akikusudia kuudanganya umma.
Jacob aliyakana mashtaka yote mawili katika kesi hiyo anayowakilishwa na Mawakili watatu akiwemo Peter Kibatala na Hekima Mwasipu.
"Upande wa mashtaka umeleta maombi wanataka Mahakama imuamuru Boni awape maafisa wa polisi wapelelezi, wachunguzi uwezo wa kuingia kwenye simu yake na mtandao wa X. Kwa hiyo tumepinga vikali maombi hayo tumesema hayana sababu , wala msingi wowote kisheria," alieleza Wakili Kibatala akizungumzia mwenendo wa kesi hiyo.
Upande wa mashtaka pia umeiomba Mahakama isimpe Boniface Jacob dhamana kwa kueleza kuwa usalama wake upo hatarini. Jambo ambalo mawakili wake wameeleza halina msingi wowote wa kisheria.
Maamuzi kuhusu dhamana ya Boniface Jacob yanategemewa kutolewa mnamo Septemba 23, 2024, saa tano asubuhi.
- Soma Pia:
Jeshi la Polisi: Tumemkamata Boniface Jacob kwa makosa ya Jinai anayotuhumiwa nayo
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga kutoa uamuzi wa dhamana Boniface Jacob, septemba 23, 2024
View: https://youtu.be/OJBOxYR_98Y?si=LwP_XXF_niPDsoaD
Waambie polisi a.k.a watekaji wawaachie vijana wetu, mazungumzo na majizi hatuhitaji.Najiuliza tu kama nikiwa mshauri wa pande mbili "kabla chai haijaisha kwenye kikombe maridhiano yatakuwa tayari".
* Kuanza upya - mambo ya nyuma hayatusaidii
Maelezo yako ni sawa na kutekwa kizembe,Boni Yai nilichojifunza hana ujasiri wowote
Taarifa anachapisha yeye halafu mahakamani anakana sio yeye ni utoto angekuwa jasiri kwelikweli Angesema ndio na niko tayari kutoa ushahidi
Hamna mtu jasiri hapo