Mwabukusi: Mbeya Sio Jiji ni Mkusanyiko wa Vijiji Vikubwa. Haina Miundombinu na Mzunguko wa Pesa ni Mdogo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
Kimsingi Kauli kama hizi hutokewa na watu wajinga na ambao wanaishi kwenye mawazo ya kale na kusikiliza stori za vijiweni zilizojaa uongo na mihemko.

Mwambukusi Toka anazaliwa Hadi anazeeka yeye Kila kitu anapinga Hadi Sasa Anatukana kwao,huu ni ugonjwa sio kawaida.

Mwambukusi anatakiwa kuelewa kwamba Yuko out of date na hana takwimu Wala data za kusema Mbeya ambayo ni kitovu Cha Uchumi wa Nyanda za Juu Kusini na Mkoa namba 3 Kwa Uchumi Mkubwa Tanzania nzima eti hauna mzunguko.

Mzunguko upi anaouzungumzia Mwambukusi? Mbeya ni kati ya Mikoa 4 ambayo wakazi wake Wana stable income Kwa mujibu wa takwimu Rasmi.

Aisha Mbeya ni kati ya Mikoa 10 inayoingiza mapato mengi TRA.Mbeya Ina Uchumi mkubwa wa dhahabu ambapo soko lake kule Chunya linaongoza Tanzania Kwa mauzo na Mapato.

Suala la miundombinu ni Changamoto ya miji yote Tanzania ikiwemo huko huko Dar anakoshinda ,lakini pia ujenzi unaendelea na mwingine umesgafanyika wa Barabara za mitaani ila Mwambukusi hafahamu zaidi ya kuponda.

View: https://www.instagram.com/p/Dbqs4ZWlow0/?igsh=MTZxcHlzazM3ZDhwdQ==
My Take
Mwambukusi anatakiwa kuelewa kwamba takribani Kila business entity iliyoko Dar pia Ina Tawi Mbeya ,kungekuwa hakuna huo mzunguko hakuna matawi ya biashara yangefunguliwa Mbeya.


Baada ya Mbukusi kupwaya Kisiasa naona anatafuta kiki Kwa kutembelea nyota ya Jiji la mbeya.
 
Haijalishi kama yupo sahihi au hayupo sahihi lakini natamani serikali ianze kufikiria hivyo, ili walete miradi ya maendeleo
Pamesahaulika sana, panakua kwa nguvu za wananchi bila mkono wa serikali
Kwani hakuna miradi? Hakuna Barabara kuu na za mitaani zinazoendelea na Ujenzi? 👇👇

Stendi kuu ,masoko ,Viwanja vya mpira vya kisasa no vyote vinajengwa.
 
Jamani tuwe wakweli mbeya kama jiji imesahaulika sana kimiundombinu. Mbeya badala ya kukua inarudi nyuma. Mwabukusi anaongelea uhalisia. Kwa sasa mbeya ndio jiji la hovyo kuliko majiji yote hapa Tanzania. Halina mvuto kabisa!
 
So ulitaka aseme uongo kwa kuwa ni kwao tu chawa? Unajuaje tatizo bila kulidefine? So Kama kwenu kuna njaa utasema kumejaa mahindi kwa kuwa tu umezaliwa humo? Au kwa baba yako kama hamna umeme utasema mnao wakati mnawasha vibatari kwa zamu kwa kuwa tu ni kwa baba yako? Chawa muwe na akili hata chembe tu mvukie barabara basi sio kila kitu hadi mlishwe na kibongosi mkariri
 
Jamani tuwe wakweli mbeya kama jiji imesahaulika sana kimiundombinu. Mbeya badala ya kukua inarudi nyuma. Mwabukusi anaongelea uhalisia. Kwa sasa mbeya ndio jiji la hovyo kuliko majiji yote hapa Tanzania. Halina mvuto kabisa!
Sasa huu ndio uongo wa kijinga.Unatakiwa kusema unataka miundombinu zaidi lakini kusema inarudi nyuma na huna facts huo ni ujinga.

Inarudi nyuma kivipi? Ngoja nikupe mfano mdogo kama uko Mbeya au hata unaijua Mbeya.Ituha kulikuwa na Lami? Ituka ilikuwepo? Kule airport iliko stendi Mpya kulikuwa na Lami? Yaani ni mifano michache kati ya mitaa kibao ambayo imewekwa mkeka.
 
Sasa zile nazo ni lami au ujinga tu ule?barabara zote mbeya ni low standard.
 
Ingawa majiji yote ya Tanzania ni vutuko ila Mbeya ni kituko zaidi kuitwa jiji.
Jiji mpaka leo hii lina nyumba za matope!
Bora hata Mbeya Ina nyumba za matope nikikuinesha vijumba vya mabanda ,mabati na majani ya migomba au tembe Dar,Arusha,Tanga na Mwanza utaita Jiji au sio Jiji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…