- Thread starter
- #161
..Chadema wamemhakikishia Adv.Mwabukusi kwamba hawakulalamika kwa OCD kwamba nyimbo za chama chao zimepigwa ktk mkutano wa Mwabukusi na wanaharakati.
Chadema inawajibu wa kuthibitisha au kukanusha lolote kutokea kokote lisilokuwa lake na kwa wakati; na hasa isilokuwa nalo maslahi.
CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni
Kwenye zama hizi za mapambano si nadra kuwa maadui wanaojinasibu overt na covert kuililia machozi ya mamba Chadema, kwamba ni machozi kuliko hata kina Lissu.
Tumesema sana haya. Hadi Yesu Kristo arudi wandugu?
Lissu rudini ubaoni, Majukwaani hakutamng'oa CCM
..Mwabukusi amesema hana tatizo lolote na Chadema na kwamba ana mahusiano mazuri nao na amewahi kufanya nao kazi nyingi kipindi cha nyuma.
Imekaa kiungwana zaidi. Tatizo ni kuwa ma CCM na vibaraka wao wengine kwa kujua au kutokujua hawataki mapatano.
Kulikoni kutokuwaelimisha hata DM huko wajumbe kama ndugu Retired ?
Ama Kwa hakika haieleweki wanafaidika nini kwenye mafarakano.
"Tunataka mapatano si mafarakano!"
Umoja ni nguvu.
..Ndio maana naendelea kusisitiza kwamba kuna jitihada za makusudi au kutokujua za kuwachonganisha Chadema na wanaharakati.
Jitihada hizo zitakuwa ni za ma CCM na vibaraka wao.
Ushauri wa bure:
Bila kujali majina, nyuso, vyeo nk vyao kokote watu hao waambiwe ukweli huo sirini na hata hadharani.