Lakini vilivyopo, si ndio hivyo tunaona vyote vimo mfukoni mwa CCM, sasa itakuwaje hapo!Hapana. Tubanane humu humu.
"Hatuhitaji utitiri wa vyama." ---JKN
Vilivyopo hakuna aliye na hati miliki.
Mwisho wa siku, hawahawa CCM watatumia nafasi ya kutokuwa na chama kuzuia harakati za kundi hili kufanya shughuli zao.
Na kwa upande wa pili, wakiunda chama ambacho wananchi watakuwa na imani nacho, na kuonekana chama chao kuwa tofauti na hawa wengine wote, kazi ya kundi hili itakuwa rahisi kuwazoa vibaraka wote wa CCM, pamoja na CCM yenyewe.
Kwa hiyo, kwa sasa, nami nashauri warasmishe shughuli zao hizi, kwa kuwa na chama.