Mwabukusi: Waziri hana Mamlaka ya kufuta Kijiji na asili ya Watu wa Ngorongoro

# RUBBISH
 
Kafanye utafiti uache bla bla Mr Stuxnet.

Wamasai hawajawahi kuwa chanzo cha Mazingira kuharibika over centuries ambazo wamekaa hapo.
Utafiti upo na huo ndiyo umwetumika kuwapunguza. Nakupa official report ya Kamishna wa Uhifadhi hapa:

"Wakati Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inaanzishwa mwaka 1959 ilikuwa na idadi ya watu wasiozidi 8,000 na mifugo isiyozidi 261,000, idadi hii ya watu kwa wakati huo ilionekana kuwa ndogo lakini iliendelea kuongezeka hadi kufikia kaya 23,889 zenye watu zaidi 100,000 na mifugo zaidi ya 850,000 (taarifa hizi ni kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022).

Ongezeko hili la watu na mifugo limekuwa changamoto kwa zaidi ya
miaka sitini toka kuanzishwa kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutokana na muingiliano wa shughuli za uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii ya watu wanaoishi ndani ya hifadhi, ili kuinusuru mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.

Serikali baada ya kupitia tafiti mbalimbali zilizofanywa na watafiti mbalimbali zote zikihusu matumizi mseto ya ardhi ya eneo la hifadhi ya ngorongoro na athari zake kwa ustawi wa mamlaka pamoja na jamii ya wananchi wanaoishi ndani ya
hifadhi serikali ya awamu ya sita ilichukua uamuzi wa busara wa kuwaelimisha wananchi wanaoishi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kuhama wao wenyewe kwa hiari kwenda maeneo mengine yaliyotengwa na serikali pamoja na sehemu nyingine wanazochagua wao wenyewe kwa ajili ya kupisha uhifadhi pamoja na kuboresha maisha yao, maeneo mahususi yaliyotengwa na serikali kwa ajili ya wananchi kuhamia ni pamoja na kijiji cha Msomera kilichopo katika wilaya ya Handeni, Saunyi wilaya ya Kilindi na Kitwai B wilaya ya Simanjiro."

(Richard Kiiza, Kamishina wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro)
 

πŸ”΄LIVE: TLS WAFUNGUKA SAKATA LA UTEKAJI NA MASAI NGORONGORO​


View: https://m.youtube.com/watch?v=0D_CSblrS5c

Mimi nina mtazamo tofauti na hawa wanasheria wetu kuhusiana na huu mgogoro....
1. Ikumbwe kuwa maeneo karibia yote yenye wanyama (National Parks, kuna kipindi huko nyuma kuna baadhi ya watu hata vijiji walilazimika kuhamishwa na kupewa maeneo mbadala ili kuyapisha yabaki kama hifadhi ya wanyama kwa faida ya watanzania wote.

2. Ninavyokumbuka kwenye historia, Wamasai waliachwa Ngorongoro kwa sababu tu walionekana hawakuwa na madhara kwa wanyama na mazingira (kipindi hicho wakiwa wachache) hivyo ilionekana kuwa, wangeendelea kuishi hapo huku wakibakia na utamaduni wao (mavazi, nyumba nk) ili kusiwe na mgogoro kati yao na wanyama/mazingira.

3. Tafasiri potofu inayo tolewa ni kuwa, Serikali inawafurusha/inawafukuza wamasai eneo lao la ngorongoro; wakati tafsiri sahihi ni kuwa, Serikali imeonesha nia ya kubadilisha matumizi ya eneo la ardhi ya Ngorongoro libakie kama mbuga ya wanyama kwa faida ya watanzania wote. Na hii imekuja kwa nia njema kwani wamasaai wameongezeka sana hivyo kuleta ukinzani kwa mazingira lakini pia maendeleo yanayo pelekea wamasai wabadilishe utamaduni wao kwa kujenga nyumba za kisasa, nk nk nk
Ikumbukwe kuwa; Serikali ingeweza kupitisha na kuanza utekelezaji wa zoezi la kuwahamisha mara moja ila badala yake, ikaona iendeshe zoezi hilo taratibu kwa maridhiano kitu ambacho, watu wenye nia ovu wamekuwa wakipotosha nia njema ya serikali.

Sijui kwanini ikifika kwa Wamasai ionekane kuwa ni tatizo na sio kwa Watanzania wengine wengi walio pisha/hamishwa maeneo yao nyakati tofauti tofauti kupisha miradi mbalimbali kwa faida ya watanzania wote?

Naona kama huu mgogoro unabebwa kwa mbeleko ila sijui ni kwa maslahi ya nani?

Mwisho japo sio kwa umuhimu; mimi sio mwanasheria ila huo ndio mtazamo wangu
 
Hizi ndio spana tulitaka

Sio blah blah za Sungusia limwana CCM
 
KUENDELEA KUKAA NA KUHARIBU UHAI WA HIFADHI HAIKUBALIKI,WAMASAI WALIO WENGI WAMEONDOKA KWA HIYARI YAO NA KWENDA MSOMERA,SASA HAO MNAOWAPIGIA KIFUA WAENDELEE KUBAKIA HAPO NI WA KUWAINGIZA KWENYE SHIDA TUH.
Tumia herufi ndogo ndogo tu mkuu utaeleweka!

Ila ujue kwamba Maalimu! Kuna mambo yatupasa tuungane ili kuwashinikiza viongozi wetu kuyaangalua upya kwa msatakabali wetu sote, yaani wao na wananchi kwa ujumla

Nadhani hakuna kosa kwenye hili Ostaz Juma au siyo?
 
βœ…βœ…βœ… HAKUNA HOJA YOYOTE ITAKAYOISHINDA HOJA YA UHIFADHI WA ENEO LA UHIFADHI WA URITHI WA KIDUNIA, NI LAZIMA WATU WAPUNGUZWE KWA LAZIMA KUNUSURU UHIFADHI, ARE THEY TREATED BAD #NO, JE KATIKA UHAMISHWAJI WAO UTU UNAZINGATIWA? #YES!
 
TLS-Ni tawi la chadema au ni kitu Gani?, tulitaraji TLS kingekuwa ni chombo cha kisheria chenye mfumo wa kitaifa tofauti kabisa imepoteza weledi wake na ni vyema IKAFUTWA KABISA, aidha ikaundwa upya chini ya kanuni maalumu, zisizotoka nje ya misingi yake ya kisheria,ingependeza kikawa ni chombo ambacho kinahoji kabla ya kudandia hoja ambazo zingine zina nia njema, kwa taifa hili.
 
Sasa si unaon report kama hii imekaa kimchongo sana.

Hapa inaongelea ongezeko la watu ambalo ni very slow and trivial for span of 60yrs.

Bado report hii haioneshi athari za kimazingira zimekuwaje
 
Haters ambao hamjui hata majukum ya kisheria ya TLS. Mnajali mkono kinywani tu......Hand To MouthπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
βœ…βœ…βœ… HAKUNA HOJA YOYOTE ITAKAYOISHINDA HOJA YA UHIFADHI WA ENEO LA UHIFADHI WA URITHI WA KIDUNIA, NI LAZIMA WATU WAPUNGUZWE KWA LAZIMA KUNUSURU UHIFADHI, ARE THEY TREATED BAD #NO, JE KATIKA UHAMISHWAJI WAO UTU UNAZINGATIWA? #YES!
Hao NEMC washawapiga stop msifukuze vinadamu.
 
Shida unatoa Chadema unaweka ccm

πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
KUENDELEA KUKAA NA KUHARIBU UHAI WA HIFADHI HAIKUBALIKI,WAMASAI WALIO WENGI WAMEONDOKA KWA HIYARI YAO NA KWENDA MSOMERA,SASA HAO MNAOWAPIGIA KIFUA WAENDELEE KUBAKIA HAPO NI WA KUWAINGIZA KWENYE SHIDA TUH.
Usiwe mwepesi wa kuonesha ujinga wako, tena kwa watu wenye uelewa.

Wamasai waliohamishiwa Tanga ni 8,000. Wamasai ndani ya Ngorongoro ni 120,000. Haya kwa hesabu inayohitaji akili ndogo kabisa, watu 120,000 ukitoa watu 8,000, wanabakia wangapi?
Kwa uwezo wako mdogo, unaona hao 8,000 ni wengi kuliko 120,000 - 8,000?
Kwa nini siku hizi idadi ya wajinga JF inazidi kuongezeka kwa kasi?
 
TLS haiwezi kufutika, utafutika wewe kwa kukosa uwezo wa akili. Viumbe wasio na akili huwa wanajifuta wenyewe.
 
Imebidi nicheke tu' πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ kwahiyo brother hao twiga na swala hawazaliani? Na kama wanazaliana wanakula wapi? Vipi mnawapelekeaga chakula kwenye parcel?

Hopeless
 
Kwa kweli tumshukuru Mungu. Kila wakati yanapokuwepo maharamia, huwainua watetezi.

Shetani ameleta majuha ya kuwapora wananchi rasilimali zao, lakini Mungu amewainua watetezi.

Tunamwomba Mungu uzidi kumlinda, kumjalia hekima, na kumpa ushindi Mwambukusi na timu yake dhidi ya maharamia wasiojali maisha ya binadamu wengine.
 
Imebidi nicheke tu' πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ kwahiyo brother hao twiga na swala hawazaliani? Na kama wanazaliana wanakula wapi? Vipi mnawapelekeaga chakula kwenye parcel?

Hopeless
THATS WHY NASEMA CHADEMA WANAWATUMIA MBUMBUMBU KAMA WAFUASI WAO UCHWARA KUTUPIGIA KELELE MITANDAONI HUMU.

TWIGA.SWALA WAKIZALIANA WANAATHIRI VIPI SHUGHULI ZA UFIHADHI??INFACT SISI TUNATAKA HAO WAMASAI WATOKE HUKO MBUGANI ILI HAO TWIGA NA SWALA WAZALIANE KWA WINGI HATA VIZAZI VIJAVYO WAJE KUNUFAIKA KAMA TUNAVYONUFAIKA SISI.

BINADAMU KWAKE SIYO MBUGANI,HAO WATAKE WASITAKE WATATOKA HUKO.
 
KUENDELEA KUKAA NA KUHARIBU UHAI WA HIFADHI HAIKUBALIKI,WAMASAI WALIO WENGI WAMEONDOKA KWA HIYARI YAO NA KWENDA MSOMERA,SASA HAO MNAOWAPIGIA KIFUA WAENDELEE KUBAKIA HAPO NI WA KUWAINGIZA KWENYE SHIDA TUH.
Kacheze mieleka mkuu
 
Kwanza inaonekana huna uelewa wa mambo haya. Ni uwongo mkubwa kudai kuwa hata mbuga nyingine za wanyama, kuna wakazi asilia waliohamishwa. Huo ni uwongo mkubwa.

Unatakiwa kwanza ufahamu jinsi hizi mbuga za wanyama na hifadhi za misitu zilivyokuwa zinapatikana. Maeneo mengi ambayo kulikuwa na wanyama wengi, wakiwemo wanyama wakali, watu walikuwa wakiyakimbia maeneo hayo. Hawakuwa wanaweka makazi. Hivyo kwa nyakati mbalimbali, Serikali ilikuwa inaweka mipaka ya hifadhi, siyo kuwahamisha wananchi ili maeneo yao yabadilike kuwa hifadhi. Kuna wakati wanadamu walikuwa wakiongezeka na kuonekana maeneo yao ya makazi na shughuli zao za kiuchumi, hayatoshi, serikali ilikuwa inabadilisha mipaka ya hifadhi kwa kupunguza eneo la hifadhi. Mara chache sana mipaka ya hifadhi ilikuwa inaongezwa kwa kumega maeneo ya vijiji na kuyaingiza kwenye hifadhi, na sababu kubwa ilikuwa kutengeneza buffer zone ili wanyama wasiuawe kiurahisi na wanadamu. Na maeneo mengi ya vijiji yaliyomegwa na kuunganishwa na hifadhi, wakati wa utawala wa Magufuri, yalirudishwa kwa wanavijiji.

Jielemishe uelewe utofauti wa kufuta makazi ya wananchi na kubadilisha mipaka. Na huko nyuma, hakujawahi kutokea eneo lolote la hifadhi eti wananchi walihamishwa toka eneo la asili na kwenda kutupwa wilaya nyingine. Leo uongozi huu wa kiharamia unawaondoa kwa nguvu wananchi kwenye maeneo yao ya asili, kuwavusha mkoa mmoja na kwenda kuwatupa mbali kabisa mkoa mwingine kwa manufaa ya mwarabu ambaye hataki wamasai wawepo eneo hilo.

Lazima wananchi wenye upendo wa kweli kwa Taifa letuna watu wake, tusimame na wamasai kuhakikisha watawala hawafanyi uharamia dhidi ya Taifa, tena kwakuwafurahisha wageni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…