Mwachie Emanuel Nchimbi punguzeni kuendesha nchi kihuni

Mwachie Emanuel Nchimbi punguzeni kuendesha nchi kihuni

Kuendesha nchi kihuni ndo kulisababisha Polepole akapotea kama unyoya. Sasa leo mnamweka kizuizini Nchimbi kwa ajili ya kulinda maslahi yenu binafsi tukisema mnaendesha nchi kihuni tunakosea? Hatuwezi kua na nchi inaendeshwa kihuni. Tangia Nchimbi amejiuzulu hakuna sehemu ambayo amejitokeza kuendelea kumshikilia naweza kusema ni hatari zaidi kama mnataka kuona hatari yenyewe endeleeni kumshikilia maana kusikia kwa Kenge mpaka damu itoke. Mnataka kuamsha hisia za watu na hasira. Mmempoteza Polepole tumekaa kimya mmeua ndugu zetu October 29 tupo kimya mmemweka jela Lissu kwa kesi za kipumbavu tuko kimya hatujasema ya mzee Ally kibao sasa kwa Nchimbi kuna kitu mnakitafuta kwa Watanzania wapenda haki na nchi yao mtakipata.
Ndio maana Tanzania inahitaji katiba mpya kuliko kitu kingine ili huu ujinga wa binadamu mmoja anapewa nguvu kubwa nakuwa Mungu mtu ufike mwisho. Imagine, Senegal raisi alimfukuza waziri wake mkuu na kufuatia katiba zinazoeleweka hivi sasa huyo waziri mkuu aliefukuzwa ndie spike wa bunge. Angalia kinachompata Nchimbi, kilichowapa akina Ndugai, Lowasa, etc. Inakuwa vita na visasi visivyokuwa na maana.
 
Leo Umesahau Gen Z walifanya Rais wa nchi kuapishwa kichochoroni Umesahau Gen Z hawa hawa waliofanya mitandaoni ya kijamii kufungwa zaidi ya siku tano Ge nZ hawa hawa waliosababisha kusimamisha shughuli zote za kiserikali siku tano bila kufanyika shughuli yoyote au Umesahau bila JWTZ bila hawa Samia hasingekua Ikulu mnasahau mapema mpaka Rais kawapa wizara unataka wawashe tena moto sema sisi ndo tuko karibu na Gen Z
Mnawa - manipulate watoto wasio na hatia wasio na uzoefu na siasa.
 
Back
Top Bottom