Mwaka 1985, Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuweka term limit kwa Rais

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Posts
501
Reaction score
1,214
Mwaka 1985 kwenye marekebisho ya katiba yetu ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuweka term limit ya vipindi viwili vya miaka mitano kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, baadaye ilifuatiwa na nchi ya Senegal kufanya hivyo

Hii ni heshima kubwa sana kwetu sisi watanzania
 
Mwaka 1985 kwenye marekebisho ya atiba yetu ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuweka term limit ya vipindi viwili vya miaka mitano kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, baadaye ilifuatiwa na nchi ya Senegal kufanya hivyo

Hii ni heshima kubwa sana kwetu sisi watanzania
Utulie uandike kwa umakini zaidi, usiwe na haraka kuleta uzi
 
Mwaka 1979 Ghana iliweka term limits ya vipindi viwili vya miaka minne kila kimoja.
Mwaka 1985 kwenye marekebisho ya katiba yetu ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuweka term limit ya vipindi viwili vya miaka mitano kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, baadaye ilifuatiwa na nchi ya Senegal kufanya hivyo

Hii ni heshima kubwa sana kwetu sisi watanzania
 
Mwaka 1979 Ghana iliweka term limits ya vipindi viwili vya miaka minne kila kimoja.

Ghana waliweka term limit ya Urais mwaka 1992, na mwaka huo ndio uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia ulifanyika nchini humo, ambapo Rais marehemu Jerry Rawlings alishinda na kuanza kutawala kidemokrasia kuanzia mwaka 1993 mpaka mwaka 2001 ambapo muda wake uliisha wa term 2 za miaka 4

Kabla ya hapo Rais Jerry Rawlings alikuwa anatawala kijeshi tangu mwaka 1979 mpaka mwaka 1992 ambapo ndio walianza kutumia katiba mpya ya kidemokrasia

Kwa hiyo sio kweli kuwa Ghana waliweka term limit za Rais mwaka 1979
 
Hilla Limann ndiye alikiwa Rais wa Ghana kati ya mwaka 1979-1981

Mwaka 1847 Liberia tayari ilikuwa na katiba yenye kuweka ukomo wa vipindi viwili kwa Rais.
Mwaka 1985 kwenye marekebisho ya katiba yetu ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuweka term limit ya vipindi viwili vya miaka mitano kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, baadaye ilifuatiwa na nchi ya Senegal kufanya hivyo

Hii ni heshima kubwa sana kwetu sisi watanzania
 
Katiba ya Comoro ya Mwaka 1978 ilikuwa na ukomo wa vipindi viwili vya Urais.
Mwaka 1985 kwenye marekebisho ya katiba yetu ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuweka term limit ya vipindi viwili vya miaka mitano kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, baadaye ilifuatiwa na nchi ya Senegal kufanya hivyo

Hii ni heshima kubwa sana kwetu sisi watanzania
 
Na imekuwa nchi ya kwanza Africa mashariki kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za Binadamu na kutofuata utawala wa Sheria - Ndani ya miaka mitano / Sita tu tumevunja record
 
Hilla Limann ndiye alikiwa Rais wa Ghana kati ya mwaka 1979-1981

Mwaka 1979 mwezi sita Kanali Jerry Rawlings alipindua serikali ya Jenerali Fred Akuffo, ambapo kanali Jerry Rawlings alianzisha kitu kinaitwa Armed Forces Revulutionary Council ( AFRC) ambapo baraza hilo la kijeshi lilikuwa na wajumbe 15, ambapo Kanali Jerry Rawlings ndio alikuwa mwenyekiti na kiongozi wa baraza hilo ambalo kimsingi ndio likikuwa linaendesha nchi

Baadaye mwezi September 1979, baraza hilo la kijeshi AFRC liliendesha uchaguzi wa kiraia ambao kimsingi haukuwa uchaguzi huru wala haukuwa uchaguzi wa kidemokrasia

Ambapo Dr Hilla Limann wa chama cha People's National Party ( PNP) kilichokuwa kinaungwa mkono na wafuasi wa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Ghana, Dr Kwame Nkrumah, alitangazwa mshindi

Dr Hilla Limann alishika madaraka ya Rais wa Ghana kama picha tu( ceremonial president) lakini kimsingi madaraka na maamuzi yote makubwa yalibaki chini ya kanali Jerry Rawlings ambaye aliendelea kuwa mwenyekiti wa baraza la kijeshi( Armed Forces Revulutionary Council)

Ndio maana miaka miwili baadaye December 1981, Jerry Rawlings alimuondoa madarakani Rais Dr Hilla Limann na chama chake cha People's National Party ( PNP) na kutangaza Provisional National Defence Council ( PNDC) kuongoza nchi kupitia military Junta na yeyeJerry Rawlings kuwa kiongozi wa kijeshi mpaka mwaka 1992 ulipofanyika uchaguzi wa kidemokrasia nchini Ghana

Kwa hiyo kimsingi Jerry Rawlings aliongoza Ghana tangu mwaka 1979 mpaka mwaka 2001
 
Mwaka 1985 kwenye marekebisho ya katiba yetu ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuweka term limit ya vipindi viwili vya miaka mitano kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, baadaye ilifuatiwa na nchi ya Senegal kufanya hivyo

Hii ni heshima kubwa sana kwetu sisi watanzania
Chadema lazima waipinge hii!
 
Hoja yako ni nini hapa?
 
Sasa ni miaka 52 toka uhuru muko madarakan mnarithishana hivyo vipindi viwili nini cha maana mumewafanyia watanzania dhidi ya matabaka ya walionacho na wasionacho, umasikini umekithiri mpaka leo mlo 1 wa chakula ni shida kwa watanzania wengi lakini ajira ni ndoto makundi ya kinyama ya watu wasiojulikana yanayoumiza watu ndio yametaradad, mahkaman hakuna haki mwenye kisu kikali ndio anakula nyama, uchumi kwenye documents mnasema umekuwa lakini umaskini uko pale pale kwa kundi la watu
 
Wagazija wana msemo usemao, ukitaka kupima mafanikio ya mtu, usiangalie kimo alichofikia, angalia urefu wa shimo aliotoka

Jamani, Tanzania ya leo sio Tanzania ya miaka30 iliyopita

Pamoja na changamoto nyingi tulizonazo sasa lakini hiyo haiondoi ukweli wa kwamba Tanzania ya sasa imepiga hatua kubwa sana katika kipindi cha miaka 59 ya uhuru
 
Back
Top Bottom