Mleta mada anatafuta namna ya kuifagilia Tanzania wakati sio kweli kwamba Tanzania ndio nchi ya kwanza katika Afrika kuweka utaratibu wa kutawala kwa mihula miwili....
Nadhani wewe ndugu yangu ndio mwenye changamoto ya kufuatilia siasa za kimataifa
Mwaka 1979 jeshi la Nigeria chini ya Jenerali Olesugun Obasanjo lilirejesha utawala wa kiraia( Nigeria second Republican) ambapo Rais Shehu Shagari alichaguliwa kuwa Rais wa jamhuri ya Nigeria, na kuanza kutawala kwa kutumia katiba ya Nigeria ya mwaka 1979, mpaka alipokuja kupinduliwa na Jenerali Muhammad Buhari mwaka 1983 mara tu baada ya kuwa ameshinda( re elected) kuongoza Nigeria kwa kipindi cha pili cha miaka 4
Lakini kama umepata muda wa kusoma iliyokuwa katiba ya Nigeria ya mwaka 1979, haikuweka term limit ya urais wa Nigeria, isipokuwa katiba hiyo ya Nigeria ya mwaka 1979, iliweka muda wa kufanya uchaguzi wa Rais ni kila baada ya miaka 4
Term limit ya Urais nchini Nigeria imekuja kuwekwa kwenye katiba yao ya mwaka 1999, kwenye sura ya sita, ibara ya 137(1)(b),ambapo imesema Rais wa Nigeria atachaguliwa kwa vipindi viwili tu, vya miaka 4, ambayo kimsingi katiba hiyo ndio inatumika mpaka sasa
Rais wa kwanza kuanza kutumia katiba hiyo ya Nigeria ya mwaka 1999, alikuwa ni Jenerali Olesugun Obasanjo, ambaye alitawala Nigeria kwa vipindi 2 vya miaka 4 kuanzia mwaka 1999 mpaka mwaka 2007
Kwa maelezo hayo machache, Nigeria waliweka term limit ya Urais kwenye katiba yao ya mwaka 1999( Nigeria Fourth Republic) na sio mwaka 1979 kama ulivyosema wewe