Mwaka 1988 siku ya kwanza kuonavideo ya wimbo Thriller wa Michael Jackson pale Drive inn sikulala usiku

Mwaka 1988 siku ya kwanza kuonavideo ya wimbo Thriller wa Michael Jackson pale Drive inn sikulala usiku

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Sitaisahau hii siku ni miaka mingi 1988 , pale Drive inn Cinema zilipo ofisi za Zantel,Msasani.

Tumetoka mtoko wa jioni na mzee wetu kuangalia filamu ambayo siikumbuki ila ninachoku.buka kabla ya filamu ulipigwa wimbo wa Thriller wa Michael Jackson

Kwa umri wangu mdogo chini ya miaka 10 yale mazombie sikulala usiku.

Drive in ndio ukumbi pekee wa cinema ambao ungeweza kuangalia filamu ukiwa ndani ya gari,mimi niliogopa nikaenda kujifungia kwenye gari.

Sasa hivi woga umenitoka ukijichanganya ninaweza kukuchinja koo
 
Sitaisahau hii siku ni miaka mingi 1988 pale Drive inn zilipo ofisi za Zantel,Msasani.

Tumetoka mtoko wa jioni na mzee wetu kuangalia filamu ambayo siikumbuki ila ninachoku.buka kabla ya filamu ulipigwa wimbo wa Thriller wa Michael Jackson

Kwa umri wangu mdogo chini ya miaka 10 yale mazombie sikukala usiku.

Drive in ndio ukumbi pekee ambao ungeweza kuangalia filamu ukiwandani ya gari,mimi niliogopanikaenda kujifungia kwenye gari.
Sasa hivi woga umenitoka ukijichanganya ninaweza kukuchinja koo
Unaendeleza utamaduni wa mzee wako kutoka na familia yake na hivyo kuacha kumbukumbu nzuri kama ulizo nazo wewe sasahivi?
 
Dah, ile ilikuwa ama 1983 ama 1984.

Pamoja an Indiana Jones katika "Raiders of the Lost Ark".

ceG9VzoRAVGwivFU403Wc3AHRys-683x1024.jpg
 
1988 nilikuwa mtu mzima
Wimbo ulitoka 1982 nakumbuka sana miaka hiyo nikiwa nimeishatoka kujitafutia maisha nje

Bora umemuenzi Mshua
Uko sahihi mkuu,,mshua alijitahidi sana kwenye swala ka familia,hongera mkuu kwa kusafiri kitambo,niaka hiyo nabaharia wakijazana pale Salamander vijana walisafiri sana kwa kuzamia meli
 
Back
Top Bottom