Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Masomo yalikua matatu tu... Lugha, Maarifa na hisabati hapo lazima utafute marks 100+ kati ya 150 ndio uanze kufikiria kupangiwa shule...

Wanafunzi walio maliza form six walipata kupiga Tempo kwenye mashule kadhaa.

Elimu bora haipo tena bongo, na siku hizi kuna vyuo vya kata ndo vimetengeneza kizazi cha ubishi kuliko kujenga hoja.
 

Kweli kabisa 2005 mambo yalibadilika kabisa kwasababu ya uwepo wa shule nyingi za kata (Zikiitwa Voda fasta/yebo yebo baadhi ya maeneo kanda ya ziwa).

Nakumbuka pia nilivyohitimu std 7 shule niliyosoma tulichaguliwa wanafunzi 20 tu, kati ya hao 20 mimi pekee ndio nilienda shule kongwe ya Serikali, waliobaki wakapelekwa shule za kata na private. Sema kuna kasifa fulani kalikuwa kanajaa kichwani[emoji23] enzi hizo.
 
Sasa mkuu enzi kulikuwa na private schools kweli au chogi
 
Mkuu umenionesha bweni langu la Kimweri hapa Tabora boys kwa chini huku uwanjani kuna choo kinanuka ukitaka kuingia lazima uvue nguo zote nje ndio uingie vinginevyo ukitoka wenzako wanakukimbia
 
1995 Ilboru secondary form 1. Yes. Ilikuwa sifa kubwa sana. Ilboru ilikuwa na wanafunzi toka tanzania nzima. Top 200 students kitaifa, 100 mzumbe, 100 ilboru. Form IV yetu ya 1998 ilishika nafasi ya kwanza tanzania nzima. Enzi hizo ukisema unasoma Ilboru, mademu wanakupapatikia tu wenyewe. Poa sana
 
Mkuu umenionesha bweni langu la Kimweri hap Tabora boys kwa chini huku uwanjani kuna choo kinanuka ukitaka kuingia lazima uvue nguo zote nje ndo uingie vinginevyo ukitoka wenzako wanakulimbia

[emoji23][emoji23], hivi kumbe hizi mambo zipo shule nyingi, nakumbuka kipindi nasoma kuna choo kimoja ulikuwa ukiingia unatundika nguo juu ya mti, vinginevyo ni hatari. Baada ya kupata huduma zinapitiliza kwenye povu[emoji23].
 
tulitoka Burka primary school tukaenda Arusha secondary school, tulikuwa saba tu kati ya watoto mia tatu ila tulivyunja rekodi
Mwaka gani hiyo mkuu?me 2003 ndiyo nimeanza form 1 hapo arusha secondary school nikitokea Naura primary school.Enzi hizo Arusha kuna shule tano tu za secondary ambazo ni Arusha sec,Arusha day,Kaloleni,Sinoni na Ilboru(hii ilikuwa ya vipaji maalumu)
 
Enzi zetu kwa Dar shule zilikuwa nne tu basi yaani Pugu,Minaki,Tambaza,Azania hakukuwapo na Benjamini Mkapa.
Mtoto wa kiume unatakiwa ukaze ili uende angalau hata Aza Boy.

Ila binafsi nilichaguliwa Ilboru kata nzima nilikuwa mwenyewe ila DsM nzima tulikuwa watatu tu.

Advance tukatupwa mzumbe pale kwa DsM tulikuwa wa tano mkoa mzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…