Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Duh! Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana (1990 kwenda nyuma). Nadhani hapo ilikuwa baada ya miaka 18 ya kufunga mkanda. Shuleni kwetu tulifaulu watoto 3 tu kati ya wanafunzi takribani 300 wa darasa la 7. Wawili kati yao, walikuwa watoto wa walimu.
 
Sisi tulifaulu watatu tu,mimi nikiwa nimewaongoza wenzangu kwa wingi wa alama nilizopata.Na pia nilikuwa mwanafunzi bora na jina langu mpaka leo lipo kwenye ubao maalumu wa majina ya wanafunzi bora kwenye ofisi ya Mwalimu mkuu.Hakika kufaulu ilikuwa ni fahari sana enzi zetu
 
Unakuta sanduku la posta hilo moja linatumiwa na watu kibao mpaka ndugu yake na rafiki yako wa kazini...
 
97 - 4 = 93 hawa wote chaaaali, doooh Tanzania yetu imetoka mbali sana mkuu
 
Kinachonifanya nipandwe na hasira ni kwamba

1.waliopata division 1 , 2 na 3 woote kwa sasa wanakuwa treated kama watu sawawaliofaulu na woote wanapangiwa shule .

2.wanaosoma vipaji maalum na wale wasiosoma vipaji maalum woote wanakuwa treated sawa means watapata mikopo woote na watakutana chuo kimoja.

3.kwa vyuoni hakuna tofauti kati ya aliyepata first class na upper second maana woote hao wanakuwa treated sawa mfano kuapply scholarship wanachukua kuanzia upper second kwenda juu.

Tanzania elimu imekufa .
 
Hahahahaaaa, eti ba'mdogo. Best siku hizi JF ninaiheshimu sana. Kuna uzi wangu wa asili ya muziki wa Zaire kuna member mule kaniambia alisoma secondary miaka ya 1970s wakati mimi nilikuwa ninamchukulia poa tu
Duh, mwambie mama watoto wako anamsalimia
 
Nilimaliza 2008 darasa la saba nakumbuka matokeo ilikua unaenda kuangalia kwa mtendaji/manispaa sina kumbukumbu vizuri pale kuna matokeo ya jumla ya wilaya yakiwa yametenganishwa kwa kila tarafa...kulikua na nyomi la watu balaaa nilipopewa matokeo kua nimefaulu Azania mtaa mzima walijua sifa kila kona dah zamani raha japo 2008 haikua mbali sana ni miaka 12 nyuma tu hapo.
 
Ni kweli zamani waliokua wanaenda private ni waliofeli au kukosa nafasi shule za serikali tofauti na sasa..na pia hata kwenye ajira wa zamani walipewanafasi waliokua wamemaliza serikalini kabla ya private
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…