Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] nimecheka maana walikuwa wanakuheshimu ujue ni kwa sababu wao walikuwa wa UPE na wewe umeenda Sekondari tena kwa kufaulu kweli kweli

2003 nilichaguliwa mwanafunzi pekee kutoka Mbozi Magharibi kwenda shule ya bweni ya Serikali zile wanaita shule za kitaifa hapo sikufuzu kwenda shule maalumu/shule za vipaji
 
Sasa hivi C mbili na D moja unaingia advance
Tena unaweza kuta C za civics na nutrition, D ya Bible/Islamic knowledge

Chuo E mbili

Akitoka hapo hataki kazi za bodaboda, eti anataka kazi za hadhi yake, hivi wana hadhi gani hawa mbwa!!!!
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Ndugu zangu waliosoma zamani kidogo itakuwa wanakumbuka vitu kama wali na maharage siku nne au tano ,wali nyama(nyama ya kuku,ng'ombe),maziwa,mikate mikubwa na siagi,uji uliochanganywa na maziwa,chai safi,madaftari na kalamu za bure,kuogelea bwawani,kula mboga za majani.........elimu imetoka mbali sana,sasa hiv ni balaa...
 
Ukweli sioni mantiki yakuwa na shule za matabaka!
Serikali irudishe tu heshima ya shule zake! Waweke mifumo itakayo chuja kuanzia top cream mpaka yule wa mwisho akasomee nini na wapi! Hii itasaidia kutengeneza ajira zisizokoma, vijana wataajiriwa na makampuni binafsi na kwa mfumo wa usawa usiohitaji vimemo! Ningeshauri serikali pia inzishe miji ya kibiashara kwa mfano ukitaka kufanya/kuajiriwa kwenye kilimo ujue chuo utakachopangiwa cha kilimo na aina ya kilimo na field ukafanyie huo mji/mkoa na uwe ndio mwanzo wa ajira/kujiajiri.
Yaani mikoa itambulike kwa biashara yake kuu Hii itaongeza pia biashara ya utalii.
Ningeshauri pia serikali isitegemee tu wataalamu waliowajiiri wapekue na mtaani watapata washauri wazuri na wakujitolea na wakaweka mambo sawa kuliko izaniavyo!
 
Serikali sikivu itakusikia
 
Sasa huo mwaka 1970 hizo private zilitoka wapi???
 
Hakika mwaka1999 darasani kwetu tuliofauru kwenda shule za bweni tulikua watatu tu .Mimi nilienda iyunga jamaa mwingine ifunda na mwingine alienda kilosa
 
Mimi nilikuwa moja ya wanafunzi 3 tuliofaulu darasa LA 7 kati ya wanafunzi 84 huko kijijini enzi hizo.niliheshimika na vijiji vyote vya kata na wote tulipelekwa special schools.
Enzi hizo elimu ikiitwa elimu.
 
Mimi nilikuwa moja ya wanafunzi 3 tuliofaulu darasa LA 7 kati ya wanafunzi 84 huko kijijini enzi hizo.niliheshimika na vijiji vyote vya kata na wote tulipelekwa special schools.
Enzi hizo elimu ikiitwa elimu.
Safi sana kaka mkubwa
 
Watano mkoa mzima sio mchezo mkuu. Na hapo ni Dar tu mkoa wa serikali, vp hiyo mikoa mingine? Si unakuta anatoka mmoja tu wa kwenda huko Mzumbe?
 
[emoji23][emoji23], hivi kumbe hizi mambo zipo shule nyingi, nakumbuka kipindi nasoma kuna choo kimoja ulikuwa ukiingia unatundika nguo juu ya mti, vinginevyo ni hatari. Baada ya kupata huduma zinapitiliza kwenye povu[emoji23].
Daaah, nyie wa boarding kiboko mkuu
 
Mwaka gani hiyo mkuu?me 2003 ndiyo nimeanza form 1 hapo arusha secondary school nikitokea Naura primary school.Enzi hizo Arusha kuna shule tano tu za secondary ambazo ni Arusha sec,Arusha day,Kaloleni,Sinoni na Ilboru(hii ilikuwa ya vipaji maalumu)
Ilboru ilikuwa maarufu sana kitaifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…