Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Najivunia wazazi wangu wote wawili kupita ktk shule hizo, na sisi watoto wao wote tumepita ktk shule hizo.
Ni faraja sana.
 
Mkuu umenionesha bweni langu la Kimweri hapa Tabora boys kwa chini huku uwanjani kuna choo kinanuka ukitaka kuingia lazima uvue nguo zote nje ndio uingie vinginevyo ukitoka wenzako wanakukimbia
Mkuu, inaonekana hicho choo ni noma sana. Vp vijana hawakukipa jina la masihara?
 
Kweli kabisa 2005 mambo yalibadilika kabisa kwasababu ya uwepo wa shule nyingi za kata (Zikiitwa Voda fasta/yebo yebo baadhi ya maeneo kanda ya ziwa).
Kanda ya ziwa hususan Mwanza na Musoma...
 
Masomo yalikua matatu tu... Lugha, Maarifa na hisabati hapo lazima utafute marks 100+ kati ya 150 ndio uanze kufikiria kupangiwa shule...

Wanafunzi walio maliza form six walipata kupiga Tempo kwenye mashule kadhaa.
Niliwahi kuomba tempo katika kampuni moja ya ulinzi kule Dar...
 
Juzi kuna. Denti nimeonana nae ni mtoto wa jirani yangu nikamuuliza kuhusu matokeo akanijibu wamefauli darasa zima kasoro mmoja nikasema kazi ipo
Tuache utani watoto wa siku hizi wanafaulu sana! kuliko sisi tuliosoma zamani....
 
Nakumbuka nilikuwa nasumbua kata nzima na kwa tarafa nakuwa wa pili au wa tatu kwenye ile mitihan tulikuwa tunafanya pamoja(nishasahau inaitwaje)

Kimbembe necta 1st selection sikuchaguliwa
Hahahahaaa pole sana mkuu kwa maana sio kwa maneno machafu ya watanzania kama ninavyowajua...
 
Kipindi hicho matokeo wanabandika ofisi ya DC. Nakumbuka baada ya kuchaguliwa kwenda secondary nilikimbilia Mwanza kwenda kufichwa kuogopa macho ya wabaya wetu maana ningerogwa. Chezea Kigoma wewe
Watani zangu WAHA wapo vizuri sana katika sekta hiyo ya kamati ya ufundi
 
Hizi shule za kata wanazoita Asante Lowassa zimesaidia kuaccomodate idadi kubwa sana ya wanafunzi kila Kata ingawa wengine hawana sifa za ufaulu.
Imesaidia sana watoto wa mama zangu wadogo kule vijijini
 
Mkuu wewe hujasema ulifaulu kwenda shule gani naona unamuongelea dada tu
 
Ni kweli
Nakumbuka baba mkubwa aliwahi nihadithia enzi hizo walichaguliwa wawili tu kwenda sekondari
Unaweza kukuta darasa la saba walikuwa hata 70 alafu wawili tu ndio walichaguliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…