Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Nakumbuka sumbawanga mjini,mwaka 2001 kurudi nyuma,ikifika disemba kabla ya christmas majina ya waliopangiwa kwenda kidato cha kwanza,manispaa nzima yanabandikwa kwenye ubao wa matangazo wa soko kuu.
Daaah, nchi imetoka mbali sana hii mkuu...
 
Mkuu hii ishu iliishia 2004 kurudi nyuma

Kuanzia 2005 alipoingia kikwete Ni mwendo wa shule za kata hata Kama ulikuwa unapasua

Nakumbuka nilipomaliza darasa la Saba shule yetu tulikuwa 232

Ila tuliochaguliwa(kufaulu) tulikuwa 14 tu wavulana Tisa na wasichana 5

Aisee tulikuwa tunaonekana watabe sana na alwatan sana kitaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Na sisi wa 2004; tumeona tusijiweke mbali,
 
Unakuta wilaya nzima kuna shule moja ya sekondari halafu shule za msingi zaidi ya120.Ilikuwa jambo la kawaida kukuta shule yote haijatoa hata mwanafunzi mmoja wa kujiunga kidato cha kwanza.

Kwa kweli aliyeleta shule za kata alifanya jambo la maana sana pamoja na changamoto zake. Kujivunia ule uzamani ambao uliwanyima wenzetu nafasi za kusoma na sababu kubwa ikiwa ni ukosefu wa shule za sekondari unakuwa sio uzalendo
Mkuu, mimi sijivunii uzamani wa watu kukosa fursa za kusoma kwa maana hata ndugu zangu wa karibu sana waliathirika na hili. Mimi ninicholenga katika mada hii ni kukumbushana wapi Tanzania yetu hii imetoka miaka hiyo ya 1990s.
 
Mkuu hii ishu iliishia 2004 kurudi nyuma

Kuanzia 2005 alipoingia kikwete Ni mwendo wa shule za kata hata Kama ulikuwa unapasua

Nakumbuka nilipomaliza darasa la Saba shule yetu tulikuwa 232

Ila tuliochaguliwa(kufaulu) tulikuwa 14 tu wavulana Tisa na wasichana 5

Aisee tulikuwa tunaonekana watabe sana na alwatan sana kitaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hapana iliisha 2007
 
Mkuu, mimi sijivunii uzamani wa watu kukosa fursa za kusoma kwa maana hata ndugu zangu wa karibu sana waliathirika na hili. Mimi ninicholenga katika mada hii ni kukumbushana wapi Tanzania yetu hii imetoka miaka hiyo ya 1990s.
Nishakuelewa mkuu, ila nilikuwa nasisitiza tu kuwa zile zama sio za kujivunia, ni maoni yangu tu kwa ujumla
 
Hivi watu wa zamani walikuwa wakiajiriwa kazini walikuwa wanajua kazi sawa na walikuwa kazini?
 
Ni kweli
Nakumbuka baba mkubwa aliwahi nihadithia enzi hizo walichaguliwa wawili tu kwenda sekondari
 
Hizi shule za kata wanazoita Asante Lowassa zimesaidia kuaccomodate idadi kubwa sana ya wanafunzi kila Kata ingawa wengine hawana sifa za ufaulu.
 
This is JF [emoji23][emoji23]
emoji23.png
emoji23.png
 
Nakumbuka nilikuwa nasumbua kata nzima na kwa tarafa nakuwa wa pili au wa tatu kwenye ile mitihan tulikuwa tunafanya pamoja(nishasahau inaitwaje)

Kimbembe necta 1st selection sikuchaguliwa

Basi hata wale mafala wakapata cha kujitetea kwa wazazi wao( utasikia " we mpaka fulan amefeli me ndio ningefaulu mtihani ulikuwa mgumu) ikawa topic

Sikutoka ndani week kadhaa nalia tu aisee sitosahau maana mzee ilibid aingilie kati kunitafutia private ndio akili ikakaa sawa
 
Nakumbuka nilikuwa nasumbua kata nzima na kwa tarafa nakuwa wa pili au wa tatu kwenye ile mitihan tulikuwa tunafanya pamoja(nishasahau inaitwaje)
Kimbembe necta 1st selection sikuchaguliwa
Vipi 2nd selection?...
 
Back
Top Bottom