Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
SCANIA 124 G hizi zilikuja chache sana.
MOja nilikuwa nayo mimi tank..
Nyingine alikuwa nayo MArehemu Steven Mchupa nayo Tank,
Tunasafiri kupeleka mafuta Geita......Lami Dar mpaka Dodoma kibao cha PEPSI..
Baada ya hapo unaanza kupiga shimo,,,ndani uko peke yako....ndio watu wachache tulioanza kusafiri peke yetu ndani ya lori...raia wakawa wanasema tunasafiri ki south....
Wengine ni Abdala KItambi huyu naye alikuwa askari full kamanda naye alikuwa anasafiri na lori kumbe shushushu...
Enzi hizo maisha barabarani yalikuwa raha sana...pia namkumbuka Omar Kurunzi huyu alikuwa super star....
Wote hawa ni watu wa SCANIA.......madereva wengine wakongwe ni Mzee Nyakunga...Edward Mpalestina....Wilson Mhema....etc etc
View: https://youtu.be/ccY936nt-ns?si=P8FH1Xz0_2H-bMC8
Hebu tueleze huyo dere kitambi kwamba alikua police na mlikuja kujuaje ,wasalaamHiyo ni imani....waungwana wapo na wa hovyo wapo
Kwanza kabisa historia yake Abdallah Kitambi alipata mafunzo CCP......Hebu tueleze huyo dere kitambi kwamba alikua police na mlikuja kujuaje ,wasalaam
Namna ipo,,,,,Kwani hakuna namna ya kisafiri naye?!
Ndio huyo huyo...... Ameendesha sana Njia ya Songea-Dar, Mbeya-DarE bwana eeh
Unamzungumzia BUrushi aliyekuwa kwenye mabasi zamani?
Aisee hatari sana mkuu kuna watu wamekula buyu huwezi wadhaniaKwanza kabisa historia yake Abdallah Kitambi alipata mafunzo CCP......
Baadae mshikaji akawa FFU.......
Halafu baadae akapatea kwenye RADA kisha akarudi katoka "Mamtoni" akawa na Coaster inamletea HESABU,(anadai alikuwa SWEDEN nyumbani kwa SCANIA).........
Huku na kule mwamba tukawa nae kwenye malori..sasa kuna siku tukiwa tunaongozana safarini tunapiga shimo mdogo mdogo usiku mkubwa, tukakutana na jamaa wametekwa mbele yetu...barabara ilikuwa imefungwa kwa mawe......Duuh Kuba babake mwamba kumbe anatembea na CHUMA kwenye gari alivyoshuka kishujaa..na kupambana na wale jamaa ni dhahiri ana mafunzo ambayo si ya kawaida.....basi baada ya pale ilibidi kufika kituo cha polisi cha Wilaya na ndipo tulipojiridhisha huyu mwenzetu si wa kawaida.....Kwa namna alivyopokelewa na Mkuu wa kituo na kwa maelezo aliyoyatoa( Lugha iliyotumika) na mwisho kupigiwa saluti........KWA KIFUPI......utamalizia mwenyewe...
N,B,
Wale majambazi(watekaji)waliuawa,,
Mashallah mashallahNdio huyo huyo...... Ameendesha sana Njia ya Songea-Dar, Mbeya-Dar