Mwaka 2020 Tsh. 10,000 ilinunua Petroli lita 5.3, leo Oktoba unaondoka na Lita 3 tu za Mafuta kituoni

Ni ushahidi tosha kwamba sasa kila mtu anazidi kuwa tajiri 'absolutely'..... japo inaweza 8siakisi utajiri 'relatively'.

Kutokana na kupanda kwa bei za vitu watu wanakuwa hawezi tena juwa na uwezo wa kuishi chini ya dola moja. Kwa hivyo watu wengi wanauvuka mstari wa utajiri wa kutupwa.

Ili kila mmoja apate hela nyingi za kununua bidhaa kwa bei kubwa itambidi kuliowa pia hela mingi matokeo yake kila mmoja anakuwa tajiri ukilinganisha na mtu wa aina hiyo miaka kumi ilopita. Ki absolute terms lakini sio relativelly nasisitiza.

Hata idadi ya wanaomiliki vyombo vinavyotumia mafuta wameongezeka sana, si magari si bodaboda. Demand ya petroli imepanda sanaaa, sasa tutategemeaje bei ibaki palepale!!!????
 
Wewe umeelewa hilo tangazo ?

Tanzania pete ni tsh 3100+.

Kwamba Zambia bei ni chini ya Tsh3100?
 
Since jiwe amefariki,graph ya TZ Kwa hela za kigeni ni mbovu sana na nchi ikakopa vya kutosha iliashangingi yaongezeke hapa ndio price fluctuation ilipoanzia tunaingiza bizaa nyingi plus mikopo kuliko tunavyozalisha hapa ndio inaua uwezo waTShs,hujiulizi kwanini wamezuia dollar?,hii ingewatia aibu kwakua uchumi upo hovyo
 
Tule kwa urefu wa kamba jamani, usinunue pikipiki kama huwezi kuweka mafuta. Tembea tu kwa miguu au panda daladala
 

Kuna mambo mengi yamebadilika. Mwaka 2020, kulikuwa na mtawala anaitwa JPM. Dola za Marekani zilikuwa sio tatizo wala hazikuwa sababu ya kuhisi kuna siku tutazitafuta kama enzi zile za uhujumu uchumi. Sijui nini kikatokea baadae...
Pili, Ukraine na Russia hawakuwa vitani. Israel na Hizbollah haikuwa that serious. Hizi vita zote zinatokea maeneo ambayo ni wazalishaji wakubwa wa mafuta. Inawezekana kabisa bei zikapanda sababu ya vita hizi.
Na la mwisho, ni ikiwezekana, lazima tuanze kutafuta jinsi ya kubadili utaratibu wa miahs. Haya mambo yataendelea kubadilika against us. Maana maisha wewe ukiwa serious kufanya mambo yamenyooka, boss wako hajari kabisa. Ana kuzoom tu
 
Watu wanaacha kutumia petroli, wapo kwenye Gas na Umeme, wewe bado umeng'ata tu?

Ng'atuka.
Inaweza kuwa anataka sana kuhamia huko ila ushuru wa kuingiza gari la umeme au la gesi, bei yake haikamatiki. Kodi bandarini zipo juu sana
 
Inaweza kuwa anataka sana kuhamia huko ila ushuru wa kuingiza gari la umeme au la gesi, bei yake haikamatiki. Kodi bandarini zipo juu sana
Siyo kweli, magari ya umeme ushuru upo chini kabisa. Hilo hilo alilona;lo anaweza kulibadili mfumo likawa la gas.

Kafanye homework yako vizuri.

Msiwe mnaongea vitu msivyovijuwa. Ni ujinga kujifanya unajuwa kumbe hujuwi. Ni heri muulize kwanza.

Kuuliza siyo ujinga.
 
Mtanikumbuka by mwendazake
 
Angalau leo diesel lita 5 kwa 15,000.
 
Hilo hilo alilona;lo anaweza kulibadili mfumo likawa la gas.

Kafanye homework yako vizuri.
Sawa mrembo, unaweza kubadili gari litumie gesi.

Utakaposafiri nalo kwa dharura kwenda kwa wazazi wako Ujiji au kwa wakwe zako Tarime, utajazia hiyo gesi wapi?
Miundombinu ipo?
 
Mnaongozwa na huyo mvaa vijora mnategemea nn
 
Ma
Magu aliwezaje Hawa wanashindwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…