Mwaka 2022 unaelekea mwisho, Malengo yako yalikuwa yapi? Umetekeleza nini? Changamoto? Let's share experience!

Mwaka 2022 unaelekea mwisho, Malengo yako yalikuwa yapi? Umetekeleza nini? Changamoto? Let's share experience!

nimejenga boma la nyumba kubwa. bado kupata ila.nyumba yangu ndogo ya kuishi ninayo.
 
Kiuchumi bado na struggle ila kielimu na kifamilia malengo yametimia.

The sun will rise again tomorrow and we will keep struggling.

#MaendeleoHayanaChama
 
Habari wakuu.

Binafsi mwaka huu niliwekea Malengo makuu matatu.

1. Kuhama nyumba ya kupanga na kuhamia kwangu (Nyumba ilikuwa hatua za mwisho yaani finishing) mungu amesaidia nimetekeleza.
2. Kuwa na eneo la ziada (plot) ambayo itakuwa kama asset ya baadaye. Nimetekeleza.
3.Kuwa na mtaji wa kuanzia 5ml Ili nije kufanya biashara ya ufuta mwakani (Hapa nimefanikiwa kukusanya 2+ml ambayo nimeihifadhi UTT AMIS - Ukwasi Ili now niweze kukuza mtaji.

NJIA ZILIZO FANIKISHA
1. Mimi ni mwajiriwa kampuni binafsi ya kahawa ipo Mbeya mshahara ni 762800 as Take home. Nasevu kila mwezi laki 3 yaani liwe jua au inyeshe mvua.

2. Nimefuga kuku wa kienyeji na nguruwe kiasi ambao kwa haraka wamenipatia faida ya almost 700,000 mpaka sasa.

3. Nalima mashamba ya kukodi ambapo nililima Maharage na viazi ambapo vimenipatia kipato cha 1,160,000 ukitoa mtaji niliotumia.

4. Allowances mbalimbali kazini.

CHANGAMOTO
Boss amekuwa taiti sana kwenye kazi yake hivyo kukosa mda wa ziada kusimamia baadhi ya miradi niliyoitaja.
2. Majungu, fitna na wivu kutoka kwa wafanyakazi wenzangu. Wanapeleka majungu kwa boss Ili waniaribie kisa viatua vicache nilivyopiga. Ila ni kawaida kwa sisi waswahili.

Mwisho naendelea kupambana kwa miezi iliyosalia ili nikamilishe palipobakia.
Una Akili nyingi kama wachaga
 
Mimi ni mwajiriwa serikalini.nilipanga Mwaka huu nihamie kwangu kutoka nyumba ya kaka.Nilijenga nyumba bado kupaua.

CHANGAMOTO.

Mwezi wa Aprili Mwaka huu bosi alinichongea Kwa mwajiri Wangu jambo zito.

Nilipoongezwa mshahara mwezi wa saba nilipanga nikope kumalizia nyumba yangu lkn mpaka Leo nimekataliwa kukopa mpaka Kesi iishe.Kesi ina mwezi wa saba sasa haijaamuliwa.Jambo hili linanipa hisia Kali ya kuachana na kazi bora nikalime
Ni kesi gani jinai au ya kinidhamu?
 
Back
Top Bottom