Mwaka 2022 utakuwa mwaka mgumu tangu nchi yetu kupata Uhuru

Mwaka 2022 utakuwa mwaka mgumu tangu nchi yetu kupata Uhuru

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Wananchi wa Tanzania, wanategemea kilimo cha mvua. Kufikia mwezi huu 12/2021 maeneo mengi ya Tanzania hakuna mvua, jua ni kali sana.

Tunaweza kuchukulia hali hii kwa namna ya kawaida. Lakini ukweli ni kwamba mwaka 2022 utakuwa mwaka mgumu sana katika nchi yetu. Ukame utakuwa mkubwa mno. Kutakuwa na ukosefu mkubwa was chakula haijawahi kutokea. Mifugo mingi itakufa. Umaskini utazikumba familia nyingi.

Sijui ni nini kinatakiwa kufanyika. Maana hali siyo shwari, hali ni ngumu mno.
 
Ni kweli mkuu hakuna mvua yaani mvua inanyesha area a afu inakaa wiki 3 au mwezi ndio inarudia tena mvua yenyewe inakuwa kidogo Sana.

Mwaka ujao ni mwaka wa njaa na Kwa mara ya kwanza nashuhudia Hali hii mikoa ya Nyanda za Juu Kusini haijawahi tokea..

Ila good enough mwaka uliopita chakula kilikuwa kingi Sana na hata sasa maghala yamejaa misosi.

Kwa mifugo sasa ndio kwisha habari yake.Tunaomba serikali ipige marufuku exports ya Mazao ya chakula,gunia la mahindi sh.60,000 saizi toka 30,000 miezi 3 iliyopita.
 
Hakuna atakayekuwa salama ndani ya nchi mwaka kesho. Jua linawaka, mahindi yanapandwa, halafu yanakauka. Mpunga ndio kabisa mandalizi bado.

Serikali ikiwatelekeza wenye njaa, basi amani itatoweka kwa sababu wataanza kukitafuta chakula kwa nguvu.

Matukio ya wizi na ujambazi yatazidi kuongezeka. Majambazi watawavamia matajiri na kuiba hela na chakula.

Mbaya zaidi, pamoja na ukame huu, bado mbolea ya kilo 50 inauzwa kwa wastani wa TSH laki moja, wakati mwaka jana ilikuwa elfu 50 huko mikoani.

Je, wizara ya kilimo na wataalamu wake wameishaanza kuwahamasisha wananchi wapande mazao yanayokomaa kwa muda mfupi na kuhimili ukame kama vile mtama na mihogo? Je, hakuna haja ya kugawa hizo mbegu bure mana wakulima hawana hela cash.

Amini usiamini, mwaka kesho tunaenda kula mtama na mihogo hadi kwa wale ambao hawajawahi kula.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kwani mwaka huu ambao mvua imenyesha kuna kaya ni tajiri zaidi ya umasikini?

Hii nchi umasikini upo kwenye sehemu kubwa sana ya familia.

Wenye nacho wataendelea kuwa nacho na masikini wataendelea kuteseka tu
 
Mahindi yanauzwa itakuwa laana ya Jiwe kuitenga nyanda za juu kusini kimaendeleo pamoja na kuleta mchango mkubwa katika taifa
 
Hakuna atakayekuwa salama ndani ya nchi mwaka kesho. Jua linawaka, mahindi yanapandwa, halafu yanakauka. Mpunga ndio kabisa mandalizi bado.

Serikali ikiwatelekeza wenye njaa, basi amani itatoweka kwa sababu wataanza kukitafuta chakula kwa nguvu.

Matukio ya wizi na ujambazi yatazidi kuongezeka. Majambazi watawavamia matajiri na kuiba hela na chakula.

Mbaya zaidi, pamoja na ukame huu, bado mbolea ya kilo 50 inauzwa kwa wastani wa TSH laki moja, wakati mwaka jana ilikuwa elfu 50 huko mikoani.

Je, wizara ya kilimo na wataalamu wake wameishaanza kuwahamasisha wananchi wapande mazao yanayokomaa kwa muda mfupi na kuhimili ukame kama vile mtama na mihogo? Je, hakuna haja ya kugawa hizo mbegu bure mana wakulima hawana hela cash.

Amini usiamini, mwaka kesho tunaenda kula mtama na mihogo hadi kwa wale ambao hawajawahi kula.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Mafisadi wanahusika vipi na ukame wenu?
Mtakao umia ni masikini tu watu wenye fedha zao hawana mashaka kabisa.
 
Haya yameongelewa toka nazaliwa Na bado tunasonga; ugumu anao mtu Na sio maisha!

Hakuna siku umekuwa Na hela ukakosa kitu, mvua haileti hela; hela tafuta, then maisha mepesi.
 
Back
Top Bottom