Mwaka 2022 utakuwa mwaka mgumu tangu nchi yetu kupata Uhuru

Mwaka 2022 utakuwa mwaka mgumu tangu nchi yetu kupata Uhuru

Umekuza mambo sana.

Mwaka 2022 hauwezi kuwa mwaka mgumu toka tumepata Uhuru.

Kuna Miaka ilikuwa ni hatari.
 
Inabidi mamlaka husika zianze kutoa tahadhari kwa wananchi wenye akiba ya chakula kutumia kwa makini akiba zao..kama hali haitabadilika ni kweli kabisa mwaka ujao utakuwa wenye changamoto sana kwenye swala la chakula.
 
Wananchi wa Tanzania, wanategemea kilimo cha mvua. Kufikia mwezi huu 12/2021 maeneo mengi ya Tanzania hakuna mvua, jua ni kali sana.

Tunaweza kuchukulia hali hii kwa namna ya kawaida. Lakini ukweli ni kwamba mwaka 2022 utakuwa mwaka mgumu sana katika nchi yetu. Ukame utakuwa mkubwa mno. Kutakuwa na ukosefu mkubwa was chakula haijawahi kutokea. Mifugo mingi itakufa. Umaskini utazikumba familia nyingi.

Sijui ni nini kinatakiwa kufanyika. Maana hali siyo shwari, hali ni ngumu mno.
Huku Dar naona mvua zinanyesha sana.
 
Hali siyo shwari. Mimi nipo huku katavi upepo wa kiangazi unapiga mwezi huu wa 12.
Na mkoa huo ndio katika mikoa yenaye neema ya mvua ni huo, sasa kama na huko ni mvua za KUDEMKA DEMKA, tumekwishaa, ila maghala mengi bado hifadhi ya chakula ipo, sema ni utaratibu gani unawekwa ili yasiuzwe nje?!!
 
Waafrika hovyo sana.Mvua imenyesha miaka 4 mfululizo tangu 2016 tumeshindwa kuweka akiba ya chakula!!
Pumbavu sana ngoja tufe.Kila mtu atafute chaka lake msitafute huruma wala mchawi. Mbozi mahind bado debe sh 7000 kanunueni muweke ndani vinginevyo ni kelele zisizokuwa na tija.
 
Tutamkumbuka Dkt Magufuli, maana angekuwepo mpaka sasa angekuwa kaanza kuweka mikakati
Magufuli hajawahi toa chakula cha bure ila kikwete.
Magufuli alikumbwa na ukame 2016 tu na aliwananga wasukuma kuwa wauze ng'ombe wanunue debe la mahindi.Alisema ni zamu ya wakulima kupata hela wauze debe la mahindi hata laki.
Usifikiri tumesahau.
 
Kutonyesha mvua kama ilivyozoeleka maeneo mengi ya nchi ni kiashiria kibaya kwa nchi iliyojawa na uongozi wa hovyo kama Tanzania, haingii akilini baada ya miaka 60 ya uhuru serikali haiwezi kununua mazao ya wakulima kwa ajili ya akiba ya chakula na kwa ajili ya soko la nje kuleta pesa za kigeni...........wakulima wanalalamika mahindi kukosa mnunuzi na hii serikali ipo kuendesha siasa za majitaka za kuua upinzani. Hii imesababisha wakulima hawaoni tija ya kulima, ukichukulia wanazidi kuongezewa bei kwenye pembejeo.....naambiwa mbolea imepanda mara mbili.​
 
kwa kweli mvua msimu huu imekata kabisa, inarashia rashia mwishoni tu mwa msimu
 
Waafrika hovyo sana.Mvua imenyesha miaka 4 mfululizo tangu 2016 tumeshindwa kuweka akiba ya chakula!!
Pumbavu sana ngoja tufe.Kila mtu atafute chaka lake msitafute huruma wala mchawi. Mbozi mahind bado debe sh 7000 kanunueni muweke ndani vinginevyo ni kelele zisizokuwa na tija.
Kama debe la mahindi Mbozi ni elfu 7, je likifika huko Kigoma litakuwa sh ngapi?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
laani ikirudie wewe
Watu wengine sijui akili zao zinawazaje, yaani anataja mahindi yasiuzwe nje ili yeye ashibe kwa gharama ndogo huku wakulima wakiumia na kutopea kwenye umaskini.
Kama vipi naye akalime auze mahindi buku 2 ili watu wasife njaa.
Mkulima ndio ngao ya njaa ya Tanzania?
Warabu wapo jangwani ika hatusikii wakilia njaa au uhaba wa mvua.
Bongo zetu hazifanyi kazi vizuri.
 
Haya yameongelewa toka nazaliwa Na bado tunasonga; ugumu anao mtu Na sio maisha!

Hakuna siku umekuwa Na hela ukakosa kitu, mvua haileti hela; hela tafuta, then maisha mepesi.
Jidanganye tu mkuu. Pesa sio kila kitu. Unaweza kuwa na Pesa ila ukakosa cha kununua. Dunia ni ngumu sana, Mungu tusaidie
 
Wananchi wa Tanzania, wanategemea kilimo cha mvua. Kufikia mwezi huu 12/2021 maeneo mengi ya Tanzania hakuna mvua, jua ni kali sana.

Tunaweza kuchukulia hali hii kwa namna ya kawaida. Lakini ukweli ni kwamba mwaka 2022 utakuwa mwaka mgumu sana katika nchi yetu. Ukame utakuwa mkubwa mno. Kutakuwa na ukosefu mkubwa was chakula haijawahi kutokea. Mifugo mingi itakufa. Umaskini utazikumba familia nyingi.

Sijui ni nini kinatakiwa kufanyika. Maana hali siyo shwari, hali ni ngumu mno.
RAMLI CHONGANISHI
 
Back
Top Bottom