Hakuna atakayekuwa salama ndani ya nchi mwaka kesho. Jua linawaka, mahindi yanapandwa, halafu yanakauka. Mpunga ndio kabisa mandalizi bado.
Serikali ikiwatelekeza wenye njaa, basi amani itatoweka kwa sababu wataanza kukitafuta chakula kwa nguvu.
Matukio ya wizi na ujambazi yatazidi kuongezeka. Majambazi watawavamia matajiri na kuiba hela na chakula.
Mbaya zaidi, pamoja na ukame huu, bado mbolea ya kilo 50 inauzwa kwa wastani wa TSH laki moja, wakati mwaka jana ilikuwa elfu 50 huko mikoani.
Je, wizara ya kilimo na wataalamu wake wameishaanza kuwahamasisha wananchi wapande mazao yanayokomaa kwa muda mfupi na kuhimili ukame kama vile mtama na mihogo? Je, hakuna haja ya kugawa hizo mbegu bure mana wakulima hawana hela cash.
Amini usiamini, mwaka kesho tunaenda kula mtama na mihogo hadi kwa wale ambao hawajawahi kula.
Sent from my TECNO F1 using
JamiiForums mobile app