Mwaka 2023 nitafia shambani, eeh Mungu nisaidie!

Sisi Vijana tunaopambana na kuamini kuwa bado tunaweza kupata mitaji shambani, Mungu wa mbinguni aendelee kutushika mkono. Binafsi nimepambana kutoka 2016 baada tu ya kuhitimu masomo yangu mwaka 2015 nikiwa nalima zao la Mahindi. Kwa bahati mbaya sana mwaka jana ndiyo ungekuwa mwaka wa mimi kutoboa lakini UKAME ukakausha mahindi almost ekari 14. NNikaishiakupata gunia 18 tu!

Sijakata ttanaamwaka huu jimeipmngia tena, ninaamini ni mwaka wangu wa kutoboa. Uzuri mahsmba ninayo mengi na ni ya bure kabisaa.

Vijana tusichoke tuendelee kupambana, nimewashuhudia vijana wengi wakitoboa kupitia kilimo. Hata mimi mwaka 2018 niliwahi kupata mahindi mengi lakini nikafanya ujinga mmoja nikijisemea kuwa acha nisubiri bei zipande.

2023 the Year of Youth in Agriculture.

Safi mkuu hakuna kukata tamaa [emoji1531]
 
Nawasalimu kwa jina la aliye juu wakulima wenzangu.

Nasimama hapa kutangaza rasmi kwamba 2023 nitafia shambani. Nimejiridha pasipo na shaka kwamba mali utaipata shambani.

Kwa hiyo 2022 nimeitumia vizuri kujiandaa na kutafuta mtaji. Nasema nitafia shambani nikijiamini kwa sababu ya maandalizi niliyofanya. Nimekuwa na zana zote muhimu za kilimo. Trekta 2 ndogo 2WD zipo tayari mguu sawa,moja ikiwa ya kulima vibarua ili mapato yake yanisaidie kuhudumia mashamba kwa ufanisi wa hali ya juu. Ile ya pili sasa itakuwa kwa ajili ya mashamba yangu tu. Tayari harrow na planter vimepatikana. Hakuna kupanda kienyeji. Ni kitaalamu tu.

Upande wa mashamba naona ni gharama sana kuyamiliki. Zimepatikana ekari 120 Singida changamoto shamba ni pori linahitaji kusafisha. Nimeziweka kiporo mwakani. Kwa hiyo mwaka huu nitakodi tu.

Kwa kuanzia nimekodi ekari 150 katika mikoa miwili tofauti. Ekari 100 zao moja ekari 50 zao lingine. Gharama za kukodi bado chini sana 40,000- 50,000. Tayari amepatikana bwana shamba ampaye nitaingia naye partnership ya mwaka mmoja kwa asilimia fulani ya mapato yote. Yeye kazi yake ni kusimamia tu kulingana na utaalamu wake. Mimi nitamuhudimia kila kitu.

Kingine nimechagua sana kutumia teknolojia. Ukiwa na hela kidogo mambo mengi yanarahisishwa na teknolojia. Kupalilia mashine zipo, kufukuza ndege mashine zipo, kupanda na kuweka mbolea zipo. Kupiga dawa nk.

Kinachobaki hapo ni kumuomba Mungu tu ashushe mvua nzuri kustawisha mazao. Mimi ni mzuri wa Risk Management, nimeona kulima mazao yanayistahili ukamu kama dengu, mtama na alizeti.

Kwa hiyo kwa upande wangu nimejitahidi na nitajitahidi sana tu, sehemu iliyobaki ni ya Baba wa Mbinguni. Wakati mvua inanyesha wewe unafurahi kupata maji ya kunywa, mimi nafurahi kuvuna maekari.

Huu ni uzi ni kwa ajili ya watu wanaoamini kufanikiwa wakimtanguliza Mungu huku wakifanya kazi. Sio wale wanamlilia Mungu bila kufanya kazi wakiamini kwenye miujiza ya bila kazi. Sio wale wakatisha tamaa kwao kila kitu kigumu.

Hatutajadili stori za kukatishana tamaa. Haimaanishi kwamba hakuna changamoto, basi tulete changamoto na mbinu za kutatua.

Kifupi 2023 tupunguze maneno meengi na ngonjera tufanye kazi.
kwakweli mwaka huu tutafia shambani kwa stress
 
Mdau VP mapambano yanaendeleaje, nlvyoona hii post niliamua kukimbilia shamba kuunga mkono vision Yako, nko napambana but nzuri nlko mvua uhakika tofauti na Amikoa mingne mvua zmekuwa haba! Tupo tunamalzia kujipatia maeneo makubwa yakiwa ktk Hali ya mapor Tena kw bei ndogo! Krbn sponges
 
Umeamua jambo jema sana.
Tafadhali sana.
Tafadhali sana.
Tafadhali sana zingatia haya.
1.Teua/chagua kwa makini sana zao/mazao utakayolima
-soko
-gharama za uzalishaji
-maarifa/utaalamu wa uzalishajj.
-changamito na utakavyozikabili.
Mfano:
*wanyama na ndege waharibifu.
*wizi (kupata usalama wa vifaa, mali na mazao.)
*usafiri na usafirishaji.
*upatikanaji wa wasaidizi (wataalamu na vibarua).
2. Mtaji wako
3. Kuwa na.muda wa usimamizi/ufuatiliaji.

Mungu akujalie na.akubariki.katika kazi hii tukufu.
 
Mdau VP mapambano yanaendeleaje, nlvyoona hii post niliamua kukimbilia shamba kuunga mkono vision Yako, nko napambana but nzuri nlko mvua uhakika tofauti na Amikoa mingne mvua zmekuwa haba! Tupo tunamalzia kujipatia maeneo makubwa yakiwa ktk Hali ya mapor Tena kw bei ndogo! Krbn sponges

Wapi huko mkuu
 
Huku kanda ya kati kilimo cha alizet msimu ujao kitakufa, bei ya mafuta imeporomoka vibaya SIRIKALI imeruhusu mabwanyenye kuingiza mafuta mbadala kutoka nje ya nchi.
Mama ameshindwa kulinda viwanda vidogo vidogo vya ndani, sad!!!.
Yaani kulinda viwanda vya ndani ndiyo mtuuzie Lita 5 ya alizeti sh elfu 40? That was too much
 
Shambani usiende kwa hisia, mwaka 2022 mimi nashukuru serikali haikupiga marufuku kuuza nje ya nchi ndio angalau nimerudisha gharama kwasababu mahindi yalikaukia shambani, nilitarajia kuvuna gunia 200 lakini nikaishia gunia 70. Nimewauzia wakenya.

Maharage nilitaka yavunwe gunia 80 lakini nimeishia kwenye 30 kwasababu kuna mvua kidogo ilileta wadudu halafu ikakata hivyo maharage karibu heka 15 yakaliwa. Mengi nilipata deal la watu wa mbegu nikawauzia. Alizeti angalau ilivumilia ukame na zipo gunia 120 nakaribia kuzikamua niuze.
Kwa hiyo umemaliza? Huna mahindi yalobaki?
 
Back
Top Bottom