Mwaka 2023 nitafia shambani, eeh Mungu nisaidie!

Maneno huumba, Kwanini unataka kufa?

Hata kama ni emphasis of matter sio Kwa namna hiyo aisee!
 
Kilimo hakilipi, huo ndio ukweli. Tena wewe kwa akili fupi ulizonazo ndio kabisaa unaangukia pua.

Narudia tena,bongo kilimo hakilipi. Kinacholipa ni udalali wa kilimo. Huo mtaji ingia vijijini nenda kalanvue kwa wakulima aalafu wewe nenda kauze hapo ndio utapata pesa

Wanalima vijijini Yale ndio maisha yao, apate akose wala hawana shida. Mwaka huu atalima ekari 5, mwakani atalima ekari 2, mwaka unaofuata ekari 7. Ndio hivyo wanaishi siku zote

Makampuni makubwa ya mazao ya biashara iwe alizeti, korosho, pamba, tumbaku n.k huwa wananunua kutoka kwa wakulima, jiulize kwa nn wao hawalimi?
 
Hapo Kazi Tu!

Heshima yako mkuu.
 
Mkubwa sikupingi lakn umenpa maswal Sana, kwa mawazo yako wakulima waliofanikiwa huwatambui? Manyara Kuna karasinga analima maelfu y hekar za ngano hanunui hata debe moja, mbeya kweny schem y umwagliaji wanakotokea ihefu fc mashamba yabanilikiwa na kampun inakima mpunga sio mchezo kwhyo wote Hawa kwako unahtimisha kw kauli kilimo hakilipi?
 
Nakubali unasema makampun makubwa y kilimo mazao y biashara hawalimi, swal kwa mim nisie na kampun nispolima napata wapi mtaj wa kununulia? Pia unajikuta unafamilia je watoto pmj na Mama yao km wanainterest na kilimo niwazuie tusubr kununua?
 
Mzee mpaka kilimo kikulipe kuna vitu vya kuzingatia.
Capital(lazima uwe na pesa)
Taarifa sahihi
Mbinu bora za kilimo
Mbegu bora
Viuatilifu na mbolea
Usimamizi mzuri
Na eneo kubwa la kutosha na zuri.

Ukiwa na hivyo vitu vyote hapo juu. Ingia shamba ukalime. Achana na habari ya kulima eka 1 sijui 2. Hizo ni za kula nyumbani. Commercial agriculture siku zote ni large scale
 
Kama utaruhusu naomba nitembelee shamba lako ili nijifunze kutokea hapo.
 
Kiberege, Ifakara, Malinyi huko kuna watu wanalima mpunga si mchezo. Dakawa hapo kwenye scheme ya mpunga watu wanalima hatari. Turiani kwenye miwa, Kilosa kwenye vitunguu, Bagamoyo kwenye mananasi, Segera kwenye mkonge. Moshi pale nadhani maeneo ya kifaru njoo hadi karibu na njia panda kilimo kinafanyika na wateja wao wengi wanatoka Kenya. Wahi asubuhi (saa 11 hadi 12 alfajiri) hayo maeneo uone Tata kibao zinazokuja beba mazao kupeleka Kenya. Maeneo yote hayo watu wamewekeza kwenye kilimo.

Ukisikia mtu anakuambia kitu flani hakilipi na bado anaendelea kukifanya, huyo tofauti na shetani ni ndogo sana([emoji16] just kidding, ila kuna ukweli ndani yake). Kama ingekua hailipi tungeacha kulima kibiashara. Hakuna binadamu alie tayari kutumia muda wake mwingi, nguvu zake nyingi, pesa zake nyingi katika kitu ambacho anajua hakina faida. Hakuna binadamu wa hivyo
 
Katika 100%, waliofanikiwa wakiwa ni 5% tu, hapo tafsiri yake nini?

Tanzania ni nchi maskini kwa sababu asilimia kubwa ni maskini, lakini haimaanishi Mo au GSM au bakhressa ni maskini

Mimi nimezungumzia majority. Kilimo hakilipi
 
Sahihi
 

Kwa hayo mazao kiongozi mfano Mahindi na maharage kwa hiyo idadi uliyotegemea kuvuna inatakiwa ulime heka ngapi kuweza kupata hiyo idadi uliyoitarajia kuvuna mkuu...?

Na utaratibu wa kuuza Kenya upoje wanakuja kuchukua huku au unawapelekea ndio unapatiwa pesa yako...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…