Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 2,209
- 4,769
Nafahamu fika kwamba, hata CCM wenyewe hawawezi kumpa kura Rais Samia.
Na kwa jinsi mambo yalivyo magumu mitaani, watu wanavyomsema, watu walivyomchoka, yeye mwenyewe anajaribu tu kuchungulia anakutana na nyuso ngumu zilizojaa hasira ya kwa nini kutufanyia hivo? Anaamua akae kimya tu.
Safari hii 2025, yeye mwenyewe hawezi kujipigia kura.
Ifahamike kuwa, kundi kubwa lililokuwa likinyanyasika ndani ya CCM na nje ya CCM kwa kusimangiwa kifo cha mpendwa wao Hayati Magufuli na kujikuta likikosa faraja likisubiri kizaliwe chama kipya kitakacholifariji kundi hilo kisitokee.
Kundi hili lilikaa kwa kukata tamaa na kuamua kuzisusa kabisa siasa za Tanzania.
Kundi hili limekuwa likishuhudia masimango kutoka karibu pande zote za vyama vya siasa. Na kwa sababu hiyo, kundi hilo lilikaa njia panda lisijuwe ni nani wa kumuunga mkono.
Katikati ya hasira hizo, CHADEMA kwa kuusoma upepo wa kisiasa, na baada tu ya tamko la M/kiti msaidizi Kusema mbele ya umma kuwa, sasa ameutambua uwezo wa Hayati Magufuli na kwamba si mwizi na pia yeye mwenyewe atadhuru kaburi lake ili akaseme jinsi wananchi wanavyonyasika ilitosha kuamsha shangwe ya kundi hilo na kurudisha matumaini kwenye chama hiko.
Kwa hali hii, CHADEMA wamejua kucheza karata.
CCM baada ya kuona hayo, nao wameanza kujutia udhalilishaji wa jina la Hayati Magufuli.
Kauli aliiyosema Prof. Mkumbo leo inaonyesha dhahiri kuwa wanamwonea wivu Tundu Lissu na CHADEMA kwa kutoa kauli ambayo imefanya kundi la Sukuma gang kuiunga mkono CHADEMA.