Mwaka huu 2023 umekupa funzo gani kubwa katika maisha yako?

Wakuu,

Mwaka 2023 unakaribia kuisha, tumekutana na mambo mengi, ya kufunza, kukatisha tamaa, kutusogeza mbele ama kuturudisha nyuma, kutupa nguvu na kutufurahisha pia.

Katika mambo yote uliyokutana nayo, ni kipi kimekugusa sana kwa namna moja ama nyingine na kukufunza jambo?
Trust..tuliowaamini sana ndio waliotuumiza sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu akikuomba chakula mpatie kama unacho, njaa ni kitu kibaya sana, heshimu fedha hata kama ni ndogo kiasi gani,. Mtu akikuomba msaada kama unaweza kumsaidia msaidie, USIMJUDGE, kama anadanganya hiyo ni juu yake.

Mfanye Mungu wako kuwa wa kwanza kwenye kila utendalo, INALIPA.

Watu wengi wako karibu na wewe kwa sababu kuna namna wanafaidishwa na vitu fulani kutoka kwako, vikiondoka HUTOWAONA, jipange kisaikolojia na wala ISIKUUMIZE.

Familia ni kila kitu kwenye maisha, Asante 2023.
 
Nimejifunza na nimesadiki ya kuwa Mungu ni mwema wakati wote, na Ukimuomba hutenda kwa wakati wake

Ni ajabu ila kweli ya kuwa asilimia karibia zote ya nilivyomwomba wakati nauanza mwaka kanitimizia nami nazidi kustaajabu juu ya miujiza na baraka zake

Hivyo sifa, utukufu, shukrani vimrejee yeye daima kwa kufanya njia pasipo njia. Amen
 
Ushauri mzuri sana huu Mkuu
 
Hongera kwa kufikia malengo Mkuu, endelea kushikilia imani yako👏
 
Kuishi Bila madeni inawezekana, kutoboa bila mkopo inawezekana. Saving inawezekana..
Hili naandika kwa ushuhuda.

Commitment ni maamuzi yasiokupendeza,
Ujinga wa kunufaisha Wakopeshaji Sitorudia tena, Itokee dharura kubwa haswa.
 
Back
Top Bottom