Mwaka huu nilipangiwa kifo, sikufa, akafa mshikaji wangu.

Si unaona mwenyewe watu wanasema ni Chai na Mandazi
 
Pole sana mkuu! Mi nadhani baadhi ya manabii wanatumia nguvu za giza, yaani akikushika tu, taarifa zote za nyuma kuhusu wewe anazipata. So ili akulimbikizie matatizo ya mbeleni kwako lazma akuaminishe kwamba anafahamu maisha yako ya nyuma.
Baadae akishakuweka kwenye ramani yake kila unalofanya ni kama ameliandaa yeye.
 
Wakati wako haujafika tu mkuu, ukifika wala hakuna kuulizana, you will perish like a fading horse!
 
Manabaa wanaotabiri mabaya na hawawezi kuyazuia sio manabii wa Mungu.
 
Dah.... Kaka nikilegea nabii mchawi atanipoteza
Huyo nabii ni mchawi kweli na anakutafuta kupitia huyo mfanyakazi mwenzako, kwenye upande wa Mungu aliyehai kazi yake ni kuokoa tu kutoka kwenye vifo vinavyopangwa kwenye ulimwengu wa giza. Kifo umekishindinda na neema ya Bwana Yesu Kristo na ushirika wa roho mtakatifu uwe pamoja nawe daima
 
Labda kama anayeua ni Babu yenu kifo utakikwepa na ikiwa anayefisha ni Allah, basi ikiandikwa tarehe Yako hapo huvuki, labda nikufahamishe unapoona sababu za kifo kwa macho Yako Kisha ukafanya juhudi za kukikwepa na ukafanikiwa jua hiyo haikuwa tarehe Yako, kwa hiyo nakuuliza hautakufa? Utakufa, kwa kifo gani? Hakuna anayejua, yaweza kuwa ajali, magonjwa, kiporomokewa, kuungua, kughariki, kupigwa, kurogwa, na sababu nyingine nyingi, hivyo fanya ibada mwabudu mola wako, KIFO NI LAZIMA usidanganywe na ndo maana ulipoambiwa ulitakiwa ufe wewe hukuwa unajua uliepukaje? Tarehe Yako bado ndugu na itafika kama ya huyo ndugu Yako na huenda tukaambiwa alitakiwa afe Fulani ukafa wewe, upuuzi elewa kifo hakikwepwi.
 
True. Nabii Sanga
 
Jiulize kwanini ulianza kupata majanga baada ya kwenda kwa huyo the so called nabii? Jibu baki nalo wewe mwenyewe
 
chenga sana huyu jamaa wanataka kuwapigia chapuo wauza mafuta na udongo.
 
Kama Kifo ni kibaya kwanini kilipangwa in the first place ? Ukizingatia unaamini kwamba aliyepanga yote ni mwema mwenye upendo na kazi yake haina makosa ?

Que Sera Sera....
 

Pole na hongera sana mkuu. Maisha yetu yako mikononi mwa bwana
 
Acha kumnyima masihi was bwana sadaka hebu weka jina na namba ya simu tutiririke!!
 
Hii ni Chai...Nabii gani afuatilie maisha ya kila aliyekuja kanisani kwake na apate muda wa kumpigia simu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…