Kushanrishathaimu
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 220
- 347
Kuna Dada mmoja tulikuwa tukifanya naye KAZI kwenye mamlaka moja ya serikali, bahati mzuri au mbaya akahamishiwa Dodoma, hivyo kituo chake cha KAZI kiko huko.
Mwaka Jana mwishoni tukiwa kwenye maandalizi ya sherehe za mwaka mpya (ambao ni huu, 2024) akanialika niende kwenye kanisa Lao lililopo Dar kwa ajili ya mkesha wa mwaka mpya, naye alikiwepo Dar likizo hiyo.
Ibada ilianza muda wa SAA mbili usiku, bendi ya Praise and worship ilikuwa ikiburudisha na kutumbuiza waumini.
Ilipofika SAA tatu usiku, ndugu Nabii alipanda jukwaani na bila kupoteza muda akaanza kutabiri randomly kwa waumini walioshiri ibada hiyo.
Mara ghafla bin vuu, akaibuka kwangu, akaniuliza, unamfahamu Butogwa? Nikajibu ndio namfahamu, akaanza kuelezea maisha ya ndugu yangu Butogwa aliyefariki mwaka 1998 tukiwa vijana wadogo.
Maelezo yake yalikuwa yamenyooka hayana mbambamba, na akapatia hadi tarehe ambayo mshikaji alitwaliwa na Bwana.
Akaendelea, Akaniambia mwaka huu hutoboi, usipokaa vizuri, kuna roho za ajali na magonjwa zinakuandama.
Miongoni mwa ajali aliyoitabiri na ikatokea vilevile ni ajali ya bodaboda, alitabiri kwamba nitakuwa tabata kwenye bata, nitapigiwa simu muhimu, nitapigiwa, nikiwa njiani nitapata ajali mbaya.
Basi mwezi wa pili siku ya St. Valentine, nilikuwa mapumziko ya kikazi, days off, nikaalikwa tabata, jamaa yangu alikuwa akimu introduce mchumba wake na kumvisha Pete.
Kwakuwa nilikuwa mapumziko, nilienda huko karamuni. Katikati ya karamu, SAA nne na nusu usiku nikapigiwa simu kutoka kwa mkurugenzi wangu akinisihi nifanye hima niende ofisini usiku huo nikaokoe jahazi.
Basi, nika request Bolt boda, iniwahishe mjini. Fasta ikaja, na mara moja safari ikaanza. Kufika maeneo ya Buguruni, dereva wa boda akaingia nyuma ya Gari ndogo, kwa spidi aliyokiwepo akarushwa hadi mbele ya Ile Gari ndogo aliyoigonga, akagonga kichwa sakafuni na kufa hapohapo, Mimi nilipata majeraha makubwa sana kichwani na sehemu nyingine za mwili. Nilipiga simu kwa mkurugenzi wangu kwamba nimepata ajali nikija kazini, nakimbizwa Amana, ajali ikaniweka bench mwezi mzima nikiwa nje ya kituo Cha KAZI.
Nikiwa najiuguza, Yule Dada wa kazini Dodoma, akanipigia simu kwamba nabii wao kaona nimepata ajali ni nimekishinda kifo na mauti.
Mwezi September 26, rafiki yangu Dr. Gilbert Sanga alifariki ghafla akiwa kazini kwake. Nabii anamtuma binti wa Dodoma anipigie simu, kwamba kuna roho ilikuwa inanizongea, lakini kwasababu Niko vizuri, imemsomba jamaa yangu.
Ajali nyingine mbaya nikipata tarehe 6 Oct, msumari wa 2½ inches uliingia kichwani baada ya kuangukiwa na Banda. Jeraha lilikuwa kubwa likiwa na urefu wa 8 inches na kina cha 2½ inches.
Nilipoteza damu nyingi sana na nilikaa tena bench mwezi mzima nikijiuguza. Nabii hakukoma kunipigia simu kwamba ameona nimepata ajali mbaya. Nikamwambia hebu achana na Mimi, sifi leo, kesho wala ntondogoo.
Namshukuru sana Mungu kwa uzima na afya na kunilinda na kunikinga na mabaya yote.
Sitakufa Bali nitaishi. Kila kwenye wingu jeusi, kuna silver line pale juu.
Dawa ni kukubali kuokoka, mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wako kisha mwombe Mungu akuoneshe kanisa ambalo watakufundisha na kukulea ili ufike mbinguni maana kufa kila mtu atakufa tu hatimaye.
Hata hivyo hizi ni siku za mwisho, wako wanaojiita manabii lakini wanatumia mapepo ya utambuzi kujua Habari za mtu. Na hili unaweza kuona kwenye Biblia, watu walitumia njia hii kujipatia kipato.
1SAMWELI 28:7
Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.
Sasa shida ni kwamba watu hawajui neno la Mungu wakiona mtu kaongea Habari zake kimiujiza na anaendesha kanisa basi hawajiulizi wanadhani ni mtumishi wa Mungu kumbe sio. Kwa maelezo yako kuna dalili huyo nabii anatumia pepo la utambuzi
Mungu kwa njia ya Roho wake huwa anamvuta mtu ili aokolewe na ukikaa vizuri na Mungu, Roho Mtakatifu atakuwa anasema na wewe mwenyewe kuhusu mambo yako huhitaji kuambiwa na mtu. Hii ni ahadi ya Yesu mwenyewe kwa wafuasi wake.
YOHANA 16:13 – 15
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.