Mwaka huu nilipangiwa kifo, sikufa, akafa mshikaji wangu.


Dawa ni kukubali kuokoka, mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wako kisha mwombe Mungu akuoneshe kanisa ambalo watakufundisha na kukulea ili ufike mbinguni maana kufa kila mtu atakufa tu hatimaye.

Hata hivyo hizi ni siku za mwisho, wako wanaojiita manabii lakini wanatumia mapepo ya utambuzi kujua Habari za mtu. Na hili unaweza kuona kwenye Biblia, watu walitumia njia hii kujipatia kipato.

1SAMWELI 28:7
Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.


Sasa shida ni kwamba watu hawajui neno la Mungu wakiona mtu kaongea Habari zake kimiujiza na anaendesha kanisa basi hawajiulizi wanadhani ni mtumishi wa Mungu kumbe sio. Kwa maelezo yako kuna dalili huyo nabii anatumia pepo la utambuzi

Mungu kwa njia ya Roho wake huwa anamvuta mtu ili aokolewe na ukikaa vizuri na Mungu, Roho Mtakatifu atakuwa anasema na wewe mwenyewe kuhusu mambo yako huhitaji kuambiwa na mtu. Hii ni ahadi ya Yesu mwenyewe kwa wafuasi wake.

YOHANA 16:13 – 15
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.

Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.
 
Hata hii post nabii keshaiona, atakupigia simu sasa hivi kabla raraa reree haja like.
 
Mpaka hapo kuna red flag nyingi tu
Hebu niwe mkweli kwa ninachowaza
Imani ni kitu kigumu sana ila kuna wakati lazima tuangalie kwa jicho la tatu
Umemuaminije mtu aliekupa historia zote mpaka vifo kama yeye ni mwema kwako?
Watu wamekufa ukiwajua na anatuma kabisa habari kwako, je hujiulizi huyu mtu ni wa aina gani?
Na je kweli kama unamuamini Mungu kwanini uamini kuwa kifo chako kimepigwa PAUSE?

Kuna watu wengi wa dini zote wanajificha kwenye Dini lakini ni washirikina wakubwa
Kama ningekuwa mimi ningemuwahi baada ya kuniambia na eti nimekwepa kifo

Ila wewe na Imani yako endelea kumfuatilia mtu anaekutafuta
 
Huyu nabii anawavua kama samaki wabichi kutoka ocean 🤣🤣🤣
 
Kwamba umeanza kupata majanga baada ya kwenda kwa huyo Nabii? Usikute yeye ndio anakutengenezea hayo majanga.
Halafu mwisho wa siku atakuambia utoe mil 5 akusafishie nyota
 
Nikapata majeraha makubwa ya kichwa na sehemu mbalimbali za mwili nikapiga simu ofisini. Hii sentensi inafikirisha.
 
Naona una mchelewesha rafiki yako wa dodoma kupata utajiri hebu kufa bhana wawaze mambo mengine
 
Mbinguni nikafanye nini? Hebu acha hizo stori soma vizuri Biblia yako.

 
Nabii hakukoma kunipigia simu kwamba ameona nimepata ajali mbaya. Nikamwambia hebu achana na Mimi, sifi leo, kesho wala ntondogoo.
Hapo ndio umenifurahisha. Kwanini iwe ana kazi ya kukufuatilia wewe tena kwenye mabalaa tu.

Ingekuwa ana kipawa kweli angeomba usikutwe na hayo majanga, ila yeye simu zake zinakuja ukishasulubika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…