Mwaka jana tarehe kama hizi, wanaCCM waliokuwa na chuki na hayati JPM walikuwa wakionyesha kebehi zao huko Twita na kuwaona Watanzania wajinga

Heading imebadilishwa na moderators hivyo haileti maana kusudiwa
 
Mimi sitasahau tarehe kama hizi alikuja kiongozi mmoja hapa mkoani akatupiga kamba hatari. Na sisi tukamwamini kutokana na eneo aliloongelea.
 
Wakati wa JK mambo yaliharibika sana.
JPM akaharibu zaidi kwa michuki yake.
Samia ndio kabisaa ni JK maradufu
Nchi bila kaudikiteta dikiteta kidogo ni ngumu sana kusimama kwenye Reli !! Watu wanataka kujitajirisha kwa njia yeyote !!
 
Watanzania wengi hawakujua kwa nini waliomchukia hayati Magufuli walikuwa wakimkebehi kupitia mitandao ya hasa Twita.

Baadhi yao wakaanza kupost picha za magari ya kijeshi yakifanya mazoezi ya parade ya kuaga mwili wa mkuu wa nchi...

Kwakweli Rais Magufuri alituharibia institution yetu na mpaka Sasa haijasimama. Tulikaa miaka mitatu na nusu bila mshahara. Kisa institution yetu haikumuunga mkono 2015. Ila tulishamsamehe.
 
Nchi zote zilizoendelea sana duniani unazozifahamu sasa- kwanza zilitawaliwa kwa mkono wa chuma ndio baadaye zikasimama kwenye Reli !! Waswahili walisemaga ukicheka na nyani utavuna mabua mkuu !!
Mkuu alistahili kuchukiwa maana si kwa ubabe sipati picha yule jamaa angeendelea hadi hivi hali ingekuwa maaana daaaah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…