Ukienda kwa msingi wa kukubali kitu kisichothibitishika kwa sababu kushindwa kuthibitisha kitu si uthibitisho kwamba hakipo, hapo itakubidi ukubali ujinga wowote ambao hauthibitishiki.
Hata mimi nikikwambia mimi ni Mungu, kwa kutumia msingi wako huo wa "kushindwa kuthibitisha kitu kipo si uthibitisho kwamba hakipo", itabidi ukubali mimi ni Mungu, kwa sababu huna jinsi ya kuthibitisha kwamba mimi ni Mungu, na mimi nitakwambia kushindwa kwako kuthibitisha kwamba mimi ni Mungu si sababu ya mimi kutokuwa Mungu. Mimi ni Mungu, wewe tu umeshindwa kuthibitisha.
Utakubali Mimi ni Mungu?
Hakuna anayeweza kuthibitisha kutokuwepo kwa kitu kisichokuwepo.
Kwa sababu kinachothibitishwa ni kilichopo, si kisichopo.
Kisichopo hakithibitishiki kutokuwapo, kwa sababu hakipo kuthibitishwa kuwa hakipo. Na kingekuwapo, kisingekuwa hakipo na hivyo kisingeweza kuthibitishika kwamba hakipo.
Thibitisha Mungu yupo.
Kwanza uko biased unakuja na pre-defined notion zako... hamna sehem nimetaj Mungu hayupo wala yupo.
Pili kama uko rational utakuwa unajua rationality huwa inabadilika kwa mda kitu kushindwa kuthibitka
leo haina maana hakitathibitka milele kisayansi.
Tatu sayansi haina scope ya kutambua ukweli wote iko limited.
nne kuiamini sayansi katika mambo yote ni imani kama imani(beliefs) zingine lakini kui-question sayansi ndio sayansi
yenyewe.
Msingi wa kufikia kusema kitu hakipo ndio mtueleze nyie smart unafikiaje hitimisho kitu hakipo na huo msingi kama
ni universal au ni personal opinion?
kipindi kile watu hawajui kama kunasayari zingine kulizifanya sayari hizo zisiwepo au wazungu walipokuja
na kusema wamegundua ziwa victoria kabla hawajagundua halikuwepo licha ya kuwa wazawa walivua samaki?
Colombus kabla ya kugundua bara la America iliyokuwa na wakazi wake iliifanya America isiwepo?
Kwa sababu sijawahi kumuona simba basi simba hayupo?
Kabla ya ugunduzi wa atom... atom haikuwepo?
mwisho kabsa unaongea opinion zako na sio fact onyesha msingi wa hoja zako sio kusema
kitu hakipo bila kusema unafikiaje hitimisho kitu hakipo.
Unakosa hoja za kisayansi unakopa philosophy ikusaidie lakini philosophy ni mtazamo tu
sio facts ndg kwa wewe rational thinker angekuwa believer philosophy ingekuwa sawa kama msingi
wa hoja zake.
Mwisho: Kajaribu kupitia scientism nini.