Mwaka Mmoja wa Kuendesha Startup: SmartBusiness – Changamoto na Mafanikio

herman3

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2015
Posts
556
Reaction score
736
Mwaka mmoja uliopita, nilianzisha program ya SmartBusiness kwa lengo moja kuu: kusaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs) barani Afrika kuboresha usimamizi biashara zao na kuwawezesha kufanya maamuzi yatokanayo na taarifa sahihi za mwenendo wa biashara zao. Niliona changamoto nyingi zinazowakabili wafanyabiashara hawa, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa solutions rahisi zinazolingana na mazingira yao, na hivyo nilitaka kuwapa suluhisho rahisi kwa gharama nafuu.

Niliyojifunza Katika Safari ya Mwaka Mmoja

Kabla ya kuanzisha SmartBusiness, nilijaribu kuanzisha startups kadhaa ambazo zilifeli ikiwemo (SafariPoa, rent finder, Online Tv, ChurchMIS, dukaPoint). Sababu kubwa ilikuwa kukosa uthabiti (consistency). Nilikuwa na mawazo mazuri, lakini changamoto za kuendesha biashara bila kujitolea vya kutosha (kutokana na kubanwa na ajira) na kushindwa kuweka juhudi za kila siku zilifanya startups hizo zishindwe kufikia malengo. Hili lilikuwa somo kubwa kwangu kuwa startup yoyote inahitaji juhudi za kila siku, hata kama hatua zinaonekana ndogo.

Hatua Kubwa ya Maamuzi (nilisema sitaki ajira tena)
Nilipoanzisha SmartBusiness, nilijua itabidi nifanye mabadiliko makubwa katika maisha yangu ili kuhakikisha mafanikio. Nilichukua uamuzi mgumu baada ya kuacha kazi yangu ya zamani tar 30 September 2023, kazi ambayo ilikuwa inanilipa zaidi ya TZS 3 milioni kwa mwezi kama take-home. Huu ulikuwa mshahara mzuri sana kwa maisha yangu, lakini niliona ili startup hii iweze kufanikiwa, nilihitaji kujitoa kikamilifu hivyo kuanzia tar 1 October 2023 nikawa jobless mwenye maono.

Nilikuwa na ndoto kubwa ya kuona SmartBusiness inasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati barani Afrika. Kwa hiyo, nikaamua kuwa full-time committed kwenye mradi huu na kuanza kufanya kazi kutoka nyumbani ili kupunguza gharama na kutumia muda wangu wote kwenye kutengeneza na kuboresha app hii. Uamuzi huu haukuwa rahisi, lakini ulikuwa na maana kubwa katika mafanikio ya mwaka huu mmoja wa SmartBusiness.

Uthabiti Ulivyobadili Kila Kitu
Kujitoa kikamilifu na kuwa thabiti
ni kitu kilichonifundisha sana. Nilipoanza kutia juhudi za kila siku—bila kujali changamoto—ndipo mambo yakaanza kubadilika. Nilijua kuwa lazima niwe consistent katika kila hatua, iwe ni kuboresha app, kutafuta wateja, au kushughulikia maoni na changamoto zao. Uthabiti huu umetufikisha mahali tulipo leo, tukiwa na zaidi ya 16,000+ downloads na kuhudumia wateja 7,000 kila mwezi kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Ghana, na Afrika Kusini.

Nimejifunza 'The Power of Small Progress'
Katika safari hii, nimejifunza kwamba kila hatua, hata kama ni ndogo, ina maana. Mafanikio hayaji ghafla, lakini hatua ndogo zinapopigwa kila siku. Kujitolea na kufanya kitu kwa moyo hata kama ni kidogo kila siku hutengeneza hatua kubwa ambayo isigefikiwa kwa mara moja. Mfano nimekuwa nikipokea maoni ya wateja tangu siku ya kwanza na kuyaweza kwenye workplan yangu ambapo nimekuwa nayavunja kwenye task ndogo Ndogo hata kama zitachukua muda mrefu kufikiwa. Kila kipengele kipya tulichoongeza kwenye SmartBusiness, kila mteja mpya tuliye mpata, kila changamoto tuliyoitatua yote hayo yametupeleka hatua moja mbele.

Kama mmiliki wa biashara jizoeze kuwa karibu na wateja
Tangu tar 17 October 2023 tarehe ambayo SmartBusiness ilikuwa published kwa mara ya kwanza nimekuwa active 24hrs kujibu request za wateja papo hapo, hii imenifanya kujua changamoto ambazo wateja wanapitia na kuzitatua kwa haraka. Hivyo imesaidia kutengeneza royal customers. Nimejifunza kuwa sababu namba moja ya wateja kuondoka kwenye biashara yako sio ubora wa bidhaa ila sababu ya kwanza ni customercare. Wakati naanzisha SmartBusiness ilikuwa na mapungufu mengi ila kwasababu ya kuwa active 24 hrs kutatua changamoto na kuwa karibu na wateja nao walifanyika sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto. Wateja wanathamini sana msaada wa haraka.

Usiwe Mfungwa wa Mipaka ya Nchi

Moja ya jambo kubwa ambalo nimejifunza ni kwamba katika biashara ya teknolojia, usifungwe na mipaka ya nchi. Teknolojia inatoa fursa za kipekee za kuvuka mipaka ya kijiografia. Ingawa SmartBusiness inaoperate kutoka Tanzania, ila tunahudumia wateja wengi kutoka Nigeria, Kenya, Uganda, na hata Afrika Kusini. Hili limekuwa somo muhimu sana kwangu, kwamba tangu siku ya kwanza naanzisha SmartBusiness vision yangu ilikuwa ni kutengeneza product ambayo itafaa kwa soko la Africa.

Kuzingatia Lengo (Focus)
Moja ya changamoto za kuendesha startup ni kutaka kufanya kila kitu kwa wakati mmoja. Lakini jambo moja nimejifunza ni umuhimu wa kuzingatia lengo kuu. Katika mwaka huu wa kwanza, tuliweka nguvu zetu katika kuhakikisha tunaboresha huduma. Hatukuacha kujaribu kila kitu, bali tulichagua maeneo ya msingi ambayo yangeweza kutupatia matokeo ya moja kwa moja.

Usifanye Kila Kitu kwa Ajili ya Pesa
Jambo jingine muhimu nililojifunza ni “usifanye kila kitu kwa ajili ya pesa.” Kila mara nilikumbana na changamoto ya kutaka kupata mapato haraka, lakini nilipofanya kazi kwa kujenga thamani kwanza, nikaona mabadiliko makubwa. Nilielewa kuwa kila biashara inahitaji kujenga thamani kwa wateja wake, kisha, pesa zitafuata.

Hii ilitufanya tuzingatie ubora wa huduma zetu na kujitahidi kutatua matatizo ya wateja wetu, na hivyo tumekuwa na wateja ambao wanatuamini na wamekuwa mabalozi wazuri wa SmartBusiness.

Watu Unaowajua Si Wateja Wako
Moja ya changamoto niliyojifunza ni kwamba watu unawajua si wateja wako. Mara nyingi, tunaweza kudhani kwamba marafiki, familia, au watu tunawajua wataamini katika bidhaa zetu. Hata hivyo, ukweli niliojifunza ni kwamba watu wengi hawaamini kuwa kitu kizuri kinaweza kutoka kwa mtu wanayemjua.

Hili ilinifanya nijipe changamoto ya kutafuta wateja wapya na kujenga uhusiano wa kudumu nao, badala ya kutegemea watu wa karibu ambao wanaweza wasiwe tayari kuamini katika bidhaa yangu. Uwezo wa kuwashawishi wateja wapya na kujenga brand ya bidhaa yetu ulikuwa muhimu kwa ukuaji wa SmartBusiness.

Hitimisho
Mwaka huu wa kwanza tunauita kama 'The year of building and Experience' kwa kuwa tumepitia uzoefu mgumu ambao startup nyingi zinakufa kwa kushindwa kuukabili.

Tutakuwa na Webinar kupitia Google Meet tarehe 17 October Muda 06:00PM. Webinar hii inafanyika katika siku ambayo SmartBusiness ilikuwa published kwa mara ya kwanza kwenye play store. Ukipenda kushiriki na kufahamu mengi kuhusu safari yetu ya mwaka mmoja jaza fomu hii ili tukutumie invitation link Join Us for the 1-Year Anniversary Webinar of SmartBusiness | 17th October 2024
 
Tangu tar 17 October 2023 tarehe ambayo SmartBusiness ilikuwa published kwa mara ya kwanza nimekuwa active 24hrs kujibu request za wateja papo hapo, hii imenifanya kujua changamoto ambazo wateja wanapitia na kuzitatua kwa haraka. Hivyo imesaidia kutengeneza royal customers. Nimejifunza kuwa sababu namba moja ya wateja kuondoka kwenye biashara yako sio ubora wa bidhaa ila sababu ya kwanza ni customercare. Wakati naanzisha SmartBusiness ilikuwa na mapungu mengi ila kwasababu ya kuwa active 24 hrs kutatua changamoto na kuwa karibu na wateja nao walifanyika sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto. Wateja wanathamini sana msaada wa haraka.

Usiwe Mfungwa wa Mipaka ya Nchi

Moja ya jambo kubwa ambalo nimejifunza ni kwamba katika biashara ya teknolojia, usifungwe na mipaka ya nchi. Teknolojia inatoa fursa za kipekee za kuvuka mipaka ya kijiografia. Ingawa SmartBusiness inaoperate kutoka Tanzania, ila tunahudumia wateja wengi kutoka Nigeria, Kenya, Uganda, na hata Afrika Kusini. Hili limekuwa somo muhimu sana kwangu, kwamba tangu siku ya kwanza naanzisha SmartBusiness vision yangu ilikuwa ni kutengeneza product ambayo itafaa kwa soko la Africa.

Kuzingatia Lengo (Focus)
Moja ya changamoto za kuendesha startup ni kutaka kufanya kila kitu kwa wakati mmoja. Lakini jambo moja nimejifunza ni umuhimu wa kuzingatia lengo kuu. Katika mwaka huu wa kwanza, tuliweka nguvu zetu katika kuhakikisha tunaboresha huduma. Hatukuacha kujaribu kila kitu, bali tulichagua maeneo ya msingi ambayo yangeweza kutupatia matokeo ya moja kwa moja.

Usifanye Kila Kitu kwa Ajili ya Pesa
Jambo jingine muhimu nililojifunza ni “usifanye kila kitu kwa ajili ya pesa.” Kila mara nilikumbana na changamoto ya kutaka kupata mapato haraka, lakini nilipofanya kazi kwa kujenga thamani kwanza, nikaona mabadiliko makubwa. Nilielewa kuwa kila biashara inahitaji kujenga thamani kwa wateja wake, kisha, pesa zitafuata.

Hii ilitufanya tuzingatie ubora wa huduma zetu na kujitahidi kutatua matatizo ya wateja wetu, na hivyo tumekuwa na wateja ambao wanatuamini na wamekuwa mabalozi wazuri wa SmartBusiness.

Watu Unaowajua Si Wateja Wako
Moja ya changamoto niliyojifunza ni kwamba watu unawajua si wateja wako. Mara nyingi, tunaweza kudhani kwamba marafiki, familia, au watu tunawajua wataamini katika bidhaa zetu. Hata hivyo, ukweli niliojifunza ni kwamba watu wengi hawaamini kuwa kitu kizuri kinaweza kutoka kwa mtu wanayemjua.

Hili ilinifanya nijipe changamoto ya kutafuta wateja wapya na kujenga uhusiano wa kudumu nao, badala ya kutegemea watu wa karibu ambao wanaweza wasiwe tayari kuamini katika bidhaa yangu. Uwezo wa kuwashawishi wateja wapya na kujenga brand ya bidhaa yetu ulikuwa muhimu kwa ukuaji wa SmartBusiness.

Hitimisho
Mwaka huu wa kwanza tunauita kama 'The year of building and Experience' kwa kuwa tumepitia uzoefu mgumu ambao startup nyingi zinakufa kwa kushindwa kuukabili.

Tutakuwa na Webinar kupitia Google Meet tarehe 17 October Muda 06:00PM. Webinar hii inafanyika katika siku ambayo SmartBusiness ilikuwa published kwa mara ya kwanza kwenye play store. Ukipenda kushiriki na kufahamu mengi kuhusu safari yetu ya mwaka mmoja jaza fomu hii ili tukutumie invitation link Join Us for the 1-Year Anniversary Webinar of SmartBusiness | 17th October 2024
BarikiwA mkuu sana i will tell same story one day
 
Japo nimeingia JF mara chache ila kwangu hii ni thread bora JF kwa kipindi hiki.
 
Big up. Uauza ujuzi wa uxoefu kwa watu wapya. Msle sure una document kila kitu na baadae taarifa hizo ziwe kitabu.
App yako inabidi uiweke wazi humu.
 
Ahsante sana, app iko public unaweza search SmartBusiness bookkeeping app kwenye app store/play store, sikutaka kuiweka link hapa kwa kuwa sikuwa na lengo la kufanya promotion ila kushirikisha uzoefu wangu huu mdogo wa mwaka mmoja
 
Mwaka mmoja uliopita, nilianzisha program ya SmartBusiness kwa lengo moja kuu: kusaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs) barani Afrika kuboresha usimamizi biashara zao na kuwawezesha kufanya maamuzi yatokanayo na taarifa sahihi za mwenendo wa biashara zao. Niliona changamoto nyingi zinazowakabili wafanyabiashara hawa, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa solutions rahisi zinazolingana na mazingira yao, na hivyo nilitaka kuwapa suluhisho rahisi kwa gharama nafuu.

Niliyojifunza Katika Safari ya Mwaka Mmoja

Kabla ya kuanzisha SmartBusiness, nilijaribu kuanzisha startups kadhaa ambazo zilifeli ikiwemo (SafariPoa, rent finder, Online Tv, ChurchMIS, dukaPoint). Sababu kubwa ilikuwa kukosa uthabiti (consistency). Nilikuwa na mawazo mazuri, lakini changamoto za kuendesha biashara bila kujitolea vya kutosha (kutokana na kubanwa na ajira) na kushindwa kuweka juhudi za kila siku zilifanya startups hizo zishindwe kufikia malengo. Hili lilikuwa somo kubwa kwangu kuwa startup yoyote inahitaji juhudi za kila siku, hata kama hatua zinaonekana ndogo.

Hatua Kubwa ya Maamuzi (nilisema sitaki ajira tena)
Nilipoanzisha SmartBusiness, nilijua itabidi nifanye mabadiliko makubwa katika maisha yangu ili kuhakikisha mafanikio. Nilichukua uamuzi mgumu baada ya kuacha kazi yangu ya zamani tar 30 September 2023, kazi ambayo ilikuwa inanilipa zaidi ya TZS 3 milioni kwa mwezi kama take-home. Huu ulikuwa mshahara mzuri sana kwa maisha yangu, lakini niliona ili startup hii iweze kufanikiwa, nilihitaji kujitoa kikamilifu hivyo kuanzia tar 1 October 2023 nikawa jobless mwenye maono.

Nilikuwa na ndoto kubwa ya kuona SmartBusiness inasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati barani Afrika. Kwa hiyo, nikaamua kuwa full-time committed kwenye mradi huu na kuanza kufanya kazi kutoka nyumbani ili kupunguza gharama na kutumia muda wangu wote kwenye kutengeneza na kuboresha app hii. Uamuzi huu haukuwa rahisi, lakini ulikuwa na maana kubwa katika mafanikio ya mwaka huu mmoja wa SmartBusiness.

Uthabiti Ulivyobadili Kila Kitu
Kujitoa kikamilifu na kuwa thabiti
ni kitu kilichonifundisha sana. Nilipoanza kutia juhudi za kila siku—bila kujali changamoto—ndipo mambo yakaanza kubadilika. Nilijua kuwa lazima niwe consistent katika kila hatua, iwe ni kuboresha app, kutafuta wateja, au kushughulikia maoni na changamoto zao. Uthabiti huu umetufikisha mahali tulipo leo, tukiwa na zaidi ya 16,000+ downloads na kuhudumia wateja 7,000 kila mwezi kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Ghana, na Afrika Kusini.

Nimejifunza 'The Power of Small Progress'
Katika safari hii, nimejifunza kwamba kila hatua, hata kama ni ndogo, ina maana. Mafanikio hayaji ghafla, lakini hatua ndogo zinapopigwa kila siku. Kujitolea na kufanya kitu kwa moyo hata kama ni kidogo kila siku hutengeneza hatua kubwa ambayo isigefikiwa kwa mara moja. Mfano nimekuwa nikipokea maoni ya wateja tangu siku ya kwanza na kuyaweza kwenye workplan yangu ambapo nimekuwa nayavunja kwenye task ndogo Ndogo hata kama zitachukua muda mrefu kufikiwa. Kila kipengele kipya tulichoongeza kwenye SmartBusiness, kila mteja mpya tuliye mpata, kila changamoto tuliyoitatua yote hayo yametupeleka hatua moja mbele.

Kama mmiliki wa biashara jizoeze kuwa karibu na wateja
Tangu tar 17 October 2023 tarehe ambayo SmartBusiness ilikuwa published kwa mara ya kwanza nimekuwa active 24hrs kujibu request za wateja papo hapo, hii imenifanya kujua changamoto ambazo wateja wanapitia na kuzitatua kwa haraka. Hivyo imesaidia kutengeneza royal customers. Nimejifunza kuwa sababu namba moja ya wateja kuondoka kwenye biashara yako sio ubora wa bidhaa ila sababu ya kwanza ni customercare. Wakati naanzisha SmartBusiness ilikuwa na mapungufu mengi ila kwasababu ya kuwa active 24 hrs kutatua changamoto na kuwa karibu na wateja nao walifanyika sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto. Wateja wanathamini sana msaada wa haraka.

Usiwe Mfungwa wa Mipaka ya Nchi

Moja ya jambo kubwa ambalo nimejifunza ni kwamba katika biashara ya teknolojia, usifungwe na mipaka ya nchi. Teknolojia inatoa fursa za kipekee za kuvuka mipaka ya kijiografia. Ingawa SmartBusiness inaoperate kutoka Tanzania, ila tunahudumia wateja wengi kutoka Nigeria, Kenya, Uganda, na hata Afrika Kusini. Hili limekuwa somo muhimu sana kwangu, kwamba tangu siku ya kwanza naanzisha SmartBusiness vision yangu ilikuwa ni kutengeneza product ambayo itafaa kwa soko la Africa.

Kuzingatia Lengo (Focus)
Moja ya changamoto za kuendesha startup ni kutaka kufanya kila kitu kwa wakati mmoja. Lakini jambo moja nimejifunza ni umuhimu wa kuzingatia lengo kuu. Katika mwaka huu wa kwanza, tuliweka nguvu zetu katika kuhakikisha tunaboresha huduma. Hatukuacha kujaribu kila kitu, bali tulichagua maeneo ya msingi ambayo yangeweza kutupatia matokeo ya moja kwa moja.

Usifanye Kila Kitu kwa Ajili ya Pesa
Jambo jingine muhimu nililojifunza ni “usifanye kila kitu kwa ajili ya pesa.” Kila mara nilikumbana na changamoto ya kutaka kupata mapato haraka, lakini nilipofanya kazi kwa kujenga thamani kwanza, nikaona mabadiliko makubwa. Nilielewa kuwa kila biashara inahitaji kujenga thamani kwa wateja wake, kisha, pesa zitafuata.

Hii ilitufanya tuzingatie ubora wa huduma zetu na kujitahidi kutatua matatizo ya wateja wetu, na hivyo tumekuwa na wateja ambao wanatuamini na wamekuwa mabalozi wazuri wa SmartBusiness.

Watu Unaowajua Si Wateja Wako
Moja ya changamoto niliyojifunza ni kwamba watu unawajua si wateja wako. Mara nyingi, tunaweza kudhani kwamba marafiki, familia, au watu tunawajua wataamini katika bidhaa zetu. Hata hivyo, ukweli niliojifunza ni kwamba watu wengi hawaamini kuwa kitu kizuri kinaweza kutoka kwa mtu wanayemjua.

Hili ilinifanya nijipe changamoto ya kutafuta wateja wapya na kujenga uhusiano wa kudumu nao, badala ya kutegemea watu wa karibu ambao wanaweza wasiwe tayari kuamini katika bidhaa yangu. Uwezo wa kuwashawishi wateja wapya na kujenga brand ya bidhaa yetu ulikuwa muhimu kwa ukuaji wa SmartBusiness.

Hitimisho
Mwaka huu wa kwanza tunauita kama 'The year of building and Experience' kwa kuwa tumepitia uzoefu mgumu ambao startup nyingi zinakufa kwa kushindwa kuukabili.

Tutakuwa na Webinar kupitia Google Meet tarehe 17 October Muda 06:00PM. Webinar hii inafanyika katika siku ambayo SmartBusiness ilikuwa published kwa mara ya kwanza kwenye play store. Ukipenda kushiriki na kufahamu mengi kuhusu safari yetu ya mwaka mmoja jaza fomu hii ili tukutumie invitation link Join Us for the 1-Year Anniversary Webinar of SmartBusiness | 17th October 2024
Tumebakiwa na siku 7, kama uko interested kuhudhuria webinar hii, usiache kujaza form hiyo
 
Back
Top Bottom