Maryam Malya
Senior Member
- Nov 29, 2021
- 116
- 260
Ipo haja kwa vyama mbalimbali vya wafanyakazi kutoa kauli ya kumpongeza Rais Samia kwa hatua alizozichukua ndani ya muda mfupi katika sekta ya utumishi wa umma, Rais ameonyesha ishara ya kujali na kuwapa watumishi wa umma kipaumbele kinachotakiwa.
Baadhi ya mambo yaliyofanywa na kutugusa watumishi moja kwa moja ni pamoja na;
1. Kupandishwa madaraja WATUMISHI laki moja tisini elfu na miatano sitini na mbili~ 190,562 (Kwa wasioelewa, hii imeigharimu Serikali kiasi cha takribani TZS BILIONI 39.6).
2. Taasisi zote zenye uhitaji wa wafanyakazi kupewa vibali vya ajira mpya na kutolewa vibali kwa watumishi walioomba kubadilisha vituo na kwenda kuongeza taaluma kwa mujibu wa taratibu na sheria za utumishi wa umma.
3. Kuanzia Mwezi March 2021 hadi January 2022, Rais Samia amewezesha ulipwaji wa madeni na malimbikizo ya watumishi wa umma wapatao 65,391, madeni yenye thamani ya takribani TZS BILIONI 90.7.
4. Kuondolewa kwa mzigo wa tozo ya 6% (VALUE RETENTION FEE) kwa watumishi waliokuwa wanufaika wa mikopo ya Elimu ya juu (HESLB). Kiwango hiki cha 6% kimekuwa mzigo mzito kwa watumishi hususani vijana wanaotoka Vyuo Vikuu, Rais Samia atakumbukwa sana kwa hili.
5. Kuboreshwa kwa mazingira ya kazi ya watumishi. Hii inatupa hamasa watumishi kutoa huduma bora na kuhakikisha wananchi wanapewa wanachostahiri.
Ingekuwa katika soka ningesema Mama yetu Samia Suluhu anaendelea kuupiga mwingi mithili ya Mreno Christian Ronaldo. Nichukue fursa hii kumpongeza Rais wetu kwa kutujali watumishi wa umma kwa vitendo.
Pia, natoa rai kwa vyama vyetu kutoa kauli za kumpongeza na kumtia moyo kiongozi huyu mwenye upendo kwetu.