Manton
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 1,163
- 1,523
Habari za wakati huu, wachambuzi makini wa masuala mbalimbali ya kunoanoa bongo; ni yangu matarajio kwamba mko salama! Naliweka swali hili mezani kutokana na kwamba nategemea kupata majibu ya kisayansi kuliko majibu yatokayo na mahaba ya kiimani na ndiyo sababu ya kuliweka jambo hili hapa na siyo kwenye jukwaa la dini.
Katika, kitabu cha Mwanzo 7:11, inaonyesha Nuhu, akiwa na miaka 600, tarehe 17 ya mwezi wa pili wa huo mwaka mvua kubwa ilianza kunyesha kwa wingi na kukoma baada ya siku 40, wakati ambapo aliendelea kukaa kwenye hiyo safina hadi maji yalipokukauka kwenye uso wa dunia, akatoka nje ya safina: Mwanzo 8:13-15, wakati Nuhu akiwa na miaka 601, tarehe 27 ya mwezi wa pili wa mwaka mwingine baada ya gharika; sawa na mwaka mmoja na siku 10 alizokaa kwenye safina tangu mvua iliponyesha na kukoma.
Sasa kwa kuwa kulikuwamo na wanyama najisi na wasafi, je, usafi ulifanyikaje, ili kuruhusu kuwepo kwa hali ya hewa nzuri, yakufanya maisha yaendelee bila bughudha wala kutia shaka kwa msomaji?