Yawezekana waliishi na uchafu wao ndani ya safina mpaka walipokuja kutoka nje!. Fikiria hili.
Umuhimu wa Usafi (hygiene) ulianza tiriwa mkazo kuanzia karne ya 19 (hapo tunaongelea miaka ya 1801s - 1900s) kabla ya hapo hakukuwa na usafi kabisa. Miji ya Paris, England, Florence, Athens unayoiona leo haikuwa misafi kabisa. Hii ilipelekea magonjwa yalioua sana watu kipindi hicho.
Watu walianza kufikiria hasa kiundani mwishoni mwa karne ya 19 kuelekea ya 20 kipindi cha
Age of Enlightenment au
Age of Reason. Hapo ndipo uelewa kuhusu masuala mbalimbali duniani, vumbuzi, na demokrasia zilipoanza kucharge bongo za watu. Soma hizi:-
1.Mwaka 430AD (kabla ya kuzaliwa Yesu) kulitokea ugonjwa uliouwa sana watu huko Athens -Ugiriki ulijulikana kama
The Plague of Athens.
2. Mwaka 165-180AD (baada ya kristo) ugonjwa mwingine ulijitokeza ukaua sana watu huko Ugiriki ulijulikana kama
The Antonine Plague nao sababu haijulikani lakini yasemekana ni uchafu. Inakadiriwa watu Millioni 5 walifariki.
3. Kufikia karne ya 14 bado watu walikuwa ni wachafu hawakuwa wamejielewa kiasi cha kufata kanuni bora za usafi. Inakadiriwa watu Millioni 50 walikufa duniani sababu ya ugonjwa fulani uliojulikana kama "
Black Death", uliambukizwa kupitia Panya, hii ni sawa na 25% - 60% ya watu wote Ulaya.
So nachotaka kukielezea hapa ni kwamba yawezekana Nuhu na wanyama waliishi na uchafu wao ndani ya safina na kwakuwa uchafu ulikuwa kitu cha kawaida kipindi chao basi hakukuwa na haja ya kuutoa nje ya safina!.
Nadharia ya Mungu kuwafunga njia za kuutoa nje ya mwili kiimani inaweza leta mantiki pia, kama aliweza leta Simba na Swala ndani ya zizi moja ashindwe vipi kufunga kutoa uchafu.
Cc:
Malcom Lumumba