Levels mzee, kuna vibarua, wafanyakazi na waajiriwa.
Ukiwa kwenye makundi mawili ya kwanza hayo ni vizuri ukapambana kujiajiri tu.
1.Vibarua hawana mikataba rasmi hawa boss akinuna akasema usije ujue ni mateso bila chuki. Mara nyingi vipato vyao havitoboi laki 3 kwa mwezi mzima. Hamna muda maalum wa kutoka kazini ila saa 12 asubuhi lazma uwepo eneo la kazi πππ na mazingira ya kazi ni magumu.
2. Wafanyakazi hawa hawana tofauti sana na vibarua isipokuwa muda wa kuripoti wengi huwa saa 2 asubuhi na kutoka saa 11 jioni na wanaenda hadi siku ya Jumamosi. Kipato chao range ni laki 5 mpaka 2M kwa waliobahatika kupata ofisi nzuri. Hawa sifa yao kuu ni kudaiwa kila kona mikopo mikopo tu alimradi. Wapo wanajitutumua na vimikebe vya mtumba toka japani na kujiona wamewin sana ila hamna kitu wanatubu sana kitaa.π
3. Wenye ajira, kiukweli ukiskia kijana amepata ajira jua tu kwamba amefanikiwa kuukimbia umaskini kwa ghafla mno kama mwanga wa radi. Hawa wengi unakuta wako kwenye Taasisi nyeti kama TCRA, TPDC, Mifuko ya hifadhi ya jamii ambako level ya mshahara si chini ya 4M kwa kuanzia tu na safari nyingi zenye per diem mlima na dili nyingi za mkwanja mrefu, hali kadhalika makampuni makubwa ya binafsi kama GGM au Barrick Gold ambako watu wanalamba 8 figures za madafu. Hawa ofisini huwa ni saa 3 mpaka saa 9 wanafunga sikuπ na benefits zote hupewa kuanzia bima kubwa ya familia, transport, communication na hata schoolfees za watoto. Hawa waajiriwa wengi ndio husukuma vyuma vya kibabe kwa 0kms na ndo juzi kwenye speech mzee wetu Jenerali ulimwengu aliwagusia kama huna disposable income walau ya 5M kwa mwezi usijitwishe gari litakutesa.
Kwahio tujichekeche tu ndugu zangu. Maswala ya kujiajiri yana mantiki kwa vibarua na wafanyakazi. Walioko kwenye level ya ajira wanaweza ku make it in life easily kuliko hata wanao hustle kupambana na kero za TRA,OSHA,FIRE, Manispaa na wengineo wengi.